Wanasiasa wa nchi za Afrika watarajia mkutano wa Dakar wa FOCAC utainua ushirikiano wa Afrika na China kwenye kiwango kipya
2021-11-26 14:45:51| CRI

Wanasiasa wa nchi za Afrika watarajia mkutano wa Dakar wa FOCAC utainua ushirikiano wa Afrika na China kwenye kiwango kipya_fororder_VCG111164225545

Mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika kuanzia Novemba 29 hadi 30 mjini Dakar, Senegal. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mawaziri wa China na nchi za Afrika kukutana ana kwa ana tangu janga la virusi vya Corona lilipolipuka, na hivyo kufuatiliwa sana na jamii ya kimataifa.

Hivi karibu, Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) liliwahoji wanasiasa na wasomi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, ambao wamesema, Baraza la FOCAC limetoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya uchumi na jamii ya Afrika katika miaka 21 iliyopita tangu lilipoanzishwa, na wanatarajia kuwa mkutano wa Dakar utaweka mipango mipya ya ushirikiano na kutia nguvu mpya kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya Afrika na China.

Katibu mkuu wa Chama tawala cha Uganda NRM Bw. Richard Awany Todwong amesema, katika miaka ya karibuni ubora wa miundombinu nchini Uganda, haswa ile ya barabara na nishati, umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na uungaji mkono wa China. Anaamini kuwa, chini ya mfumo wa FOCAC, Afrika na China zitaendelea kuimarisha ushirikiano kwenye sekta za uchumi na biashara, utalii, kilimo na rasilimali watu, na kusukuma mbele ushirikiano huo ufikie ngazi ya juu zaidi.

Msemaji wa serikali ya Uganda Bw. Ofwono Opondo anaona kuwa, kuibuka wa China kunabeba matumaini ya Afrika, kwa kuwa dhana ya China ni kusukuma mbele ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja, ambayo itanufaisha binadamu wote. Bw. Opondo anatumai kuwa mkutano wa Dakar utafuatilia zaidi miradi ya miundombinu ya kuvuka mipaka ya nchi, ili kuchangia zaidi mafungamano na munganiko kati ya nchi za Afrika.

Naibu spika wa Bunge la Afrika Kusini Bw. Solomon Lechesa Tsenoli amesema, kama nchi nyingine nyingi za Afrika, Afrika Kusini pia imenufaika na mawasiliano na ushirikiano kati yake na China, haswa kwenye ujenzi wa uwezo na maendeleo ya viwanda. Bw. Tsenoli amesema, wakati utekelezaji wa Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA) umeanza rasmi mwaka huu, kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na China na kati ya Kusini na Kusini kuna umuhimu mkubwa. Amesema, anatarajia kuwa kupitia msaada wa China, Afrika itaweza kuinua zaidi uwezo wake wa utengenezaji wa bidhaa viwandani na kuharakisha mchakato wa maendeleo ya viwanda. Anatumai kuwa ushirikiano kati ya Afrika na China utaendelea kunufaisha watu wa pande hizo mbili.

Naibu mkuu idara ya habari maelezo Tanzania Bw. Rodney Mbuya amesema, kilicholetwa na FOCAC ni ushirikiano wa kunufaishana, ambapo mazao ya kilimo ya Tanzania yamepata fursa ya kuingia kwenye soko la China, huku kampuni za China zikiwa mkandarasi muhimu wa miradi ya ujenzi nchini Tanzania. Anatarajia kuwa mkutano wa Dakar utaunganisha zaidi ajenda ya ushirikiano wa Afrika na China na Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika.