Waafrika wapongeza matokeo ya mkutano wa mawaziri wa FOCAC
2021-12-03 09:18:24| CRI

Waafrika wapongeza matokeo ya mkutano wa mawaziri wa FOCAC_fororder_fb28f9594eb844189d5169308cc9d9c4

Kongamano la majopo ya kimataifa ya washauri bingwa kuhusu matokeo ya mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) limefanyika hivi karibuni, na wajumbe kutoka Afrika wamepongeza matokeo yaliyopatikana kwenye mkutano huo, na kueleza matumaini yao kuhusu utekelezaji wa miradi husika.

Mtendaji mkuu wa idara ya maendeleo ya Umoja wa Afrika anayeshughulikia uhusiano mpya wa wenzi wa maendeleo ya Afrika Ibrahim Assane Mayaki, ameipongeza China kwa kuahidi kutoa dozi nyingine bilioni moja za chanjo ya COVID-19 kwa Afrika, na kusema hatua hiyo inaonesha nia ya China ya kushirikiana na Afrika katika kupambana na janga la COVID-19.

Balozi wa Umoja wa Afrika nchini China Rahamtalla Mohamed Osman, amesema mkutano huo umekuwa na matokeo mengi, na kuanzisha sekta mpya za ushirikiano kati ya Afrika na China.

Waziri wa zamani wa uchumi na fedha wa Guinea Malado Kab ameipongeza zaidi China kwa kuahidi kuongeza uwekezaji katika miundombinu barani Afrika, kwani anaona Afrika inahitaji uwekezaji zaidi katika miundombinu ili kupata maendeleo.