Wasomi wa China na Afrika wapongeza matokeo ya mkutano wa nane wa mawaziri wa FOCAC
2021-12-03 15:55:56| CRI

Wasomi wa China na Afrika wapongeza matokeo ya mkutano wa nane wa mawaziri wa FOCAC_fororder_M0M}5U3F_6U$]CWB07U5~GD

Wasomi kutoka China na nchi za Afrika wamepongeza matunda yaliyopatikana kwenye mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofungwa Novemba 30 huko Dakar, katika kongamano maalumu lililoandaliwa jana Alhamisi na Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo kikuu cha ualimu cha Zhejiang.

Wasomi wa China na Afrika wapongeza matokeo ya mkutano wa nane wa mawaziri wa FOCAC_fororder_V3JA_{7(L$X~WIKB%8TDX6L

Akifungua kongamano hilo, mkurugenzi wa taasisi hiyo profesa Liu Hongwu amesema, nyaraka nne zilizotolewa na “Miradi Tisa” ya ushirikiano iliyotangazwa kwenye mkutano huo, vyote vimeonesha kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika utazingatia zaidi kukidhi mahitaji halisi ya nchi za Afrika, na kuendana zaidi na maslahi ya maendeleo ya nchi hizo. Amesema ushirikiano wa China na Afrika si kama tu umetangulia mbele kwenye ushirikiano wa dunia na Afrika, na bali pia umekuwa mfano wa kuigwa kwenye ushirikiano wa Kusini-Kusini.

Wasomi wa China na Afrika wapongeza matokeo ya mkutano wa nane wa mawaziri wa FOCAC_fororder_)R(8FZ6P[}@10E}810`NL}C

Akihutubia kongamano hilo, mtafiti mwandamizi wa taasisi hiyo Bw. Gert Johannes Grobler ambaye alikuwa balozi wa Afrika Kusini katika nchi za nje, amesema mkutano huo wa FOCAC ambao umeleta matokeo ya pande zote yanayopimika, kutekelezeka na kutupia macho siku za baadaye, umetajwa na viongozi wa Afrika kuwa “mafanikio kamili”, na utaratibu wa FOCAC unazidi kuwa mfano wa kuigwa kwenye ushirikiano wa kimataifa.

Naye katibu mkuu wa kamati ya chama cha CPC ya taasisi hiyo profesa Wang Heng ambaye pia alihudhuria kongamano hilo amesema, matunda yaliyopatikana kwenye mkutano wa Dakar yamedhihirisha mara nyingine tena kuwa kushikilia maendeleo ya kijani ni dhana muhimu ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na mradi wa maendeleo ya kijani umeorodheshwa kuwa miongoni wa Miradi Tisa katika awamu yake ya kwanza ya miaka mitatu ijayo kwenye Ajenda ya Ushirikiano kati ya China na Afrika ya 2035 iliyotungwa kwa pamoja na pande hizo mbili. Amesema China na nchi za Afrika zinapaswa kutekeleza wajibu kwenye suala la mabadiliko ya tabianchi kulingana na kiwango chao cha maendeleo na hali halisi ya nchi zao, na kuendeleza mawasiliano na ushirikiano kwenye mambo ya sera, miradi na utafiti, ili kusukuma mbele juhudi za kuboresha usimamizi wa mazingira na kuhimiza maendeleo endelevu katika China na Afrika.

Wasomi na wataalamu 13 kutoka China na nchi za Afrika zikiwemo Nigeria, Cameroon na Somalia, walitoa hotuba kwa njia ya video kwenye kongamano hilo.