Safari siku ya pili

cri 2011-09-18 11:54:07

Na Chris Wa'ngombe

Shughuli siku ya pili zilianza pale tulipokuwa na sherehe za kuanzisha rasmi zoezi hili la kunasa mila desturi na hata tabiaza wenyeji pamoja na wakazi wa Xinjiang mashuhuri kama "Xinjiang through mylens". Sherehe hiyo iliyokuwa ya kufana sana ilihudhuriwa na naibu mkuu wachina redio kimataifa Bi Wang Dongmei.

Shughuli ilipotamatishwa basi tukaanza safari hadi eneo hifadhi la Tianchi. Eneo maarufu kwamandhari yake nzuri kutokana na jitihada za serikali ya mkoa pamoja na wakazi kuhifadhi eneo hilo. Kwetu sisi wageni kutoka nchi mbali mbali kutembea kwetukulituwezesha kufurahia pamoja na kujifunza mengi kuhusu uhifadhi wa mazingira. Nyumbani kenya uhifadhi wa mazingira ni swala ambalo linapewa kipao mbelekutokana na kutegemea kwetu kwa mvua ili kufanikisha kilimo pamoja nauzalishaji wa kawi. Haswa wakati huu ambao uchumi wa taifa unatarajiwa kuzidikukua, ni jambo ambalo kwa kweli linatoa funzo muhimu kwangu na hata marafikiwangu kutoka nchi geni. Hii sio kusema kuwa safari yetu haikuwa na changa motokwangu haswa. Hii ni kutokana na kijibaridi kingi ambacho kilitokana na kuwaeneo hili ni la milima, lakini sikusazwa. Kwa kuwa ni mara ya kwanza kutembeleaeneo kama hili na pia kutokana na ukarimu wa wenyeji wa tianshi basi ilinibidinipige moyo konde na kuendelea na shughuli za ziara. Mwanadada, ambaye nimakalimeni wetu sisi kundi la kiswahili kutoka kenya, Han Mei pia naye hakuchoka kujibu maswali yetu mengi kuhusu eneo hili lauhifadhi wala kututembeza hadi tukatosheka na yale tuliyoyaona. Kwa kweli haiwezekani kuzuru eneo hili lote kwa siku moja kwani eneo la Tianshi ni eneoambalo ni kubwa sana. Eneo ambalo linajumuisha milima, mabonde huku miti ikimeapande zote na hata ziwa liliomo katikati mwa hifadhi likiwa vutio kubwa kwawananchi wa jamhuri ya uchina. Hata kama kila siku wengi hutembelea eneo hiliwageni huheshimu sana hifadhi hii na kutokana na haya hifadhi hii haijaharibiwa kutokana na kuwa wageni wengi hufzuru eneo hili. Funzo kubwa kwanguni umuhimu wa kuhifadhi mazingirakwasababu ya kizazi kijapo na pia funzotunalopata kutoka mazingira kuhusu faida tunazopata kutokana na kuwekeza zaidi mbinu za uhifadhi. Changamoto kwetu kama wakenya na hata wakaazi wa afrika kwa jumla ni kubuni njia mpya za kuhifadhi mazingira na hata kujumuisha umma kwa kazi hii muhimu. Haya basikesho pia ni siku, karibu tupate kuyajua mengi kuhusu Xinjiang.