Safari ya Turpan

cri 2011-09-18 12:01:04

Na Chris Wa'ngombe

Niha..salamu kwa lugha ya kichina. Leo ilikuwa ni siku yetu ya tatu mjini Urumqi. Siku ambayo ilikuwa na shughuli tele. Tulianza majira ya saa tatu tukielekea kilomita mia moja tisaini namoja safari ambayo ilitufikisha katika eneo la Turpan. Hapa tuliweza kuona mojawapo wa namna mkoa wa Xinjiang unabuni kawi. Mbinu zinazotumika ni kwa kutumia vijito eneo ambalo linazidi ekari mia moja linatumika kwa shughuli hii huku eneo la mradi huo ukizidi kupanuliwa. Kando ya vijito hivyo ni ziwa ambalo linatumiwa kuvuna chumvi inayotumika katika mkoa huu na maeneo mengine nchini China. Ni muhimu kuelewa kuwa mahitaji ya mkoa wa Xinjiang kwa utumizi wa kawi ni muhimu sana kwa kufanikisha miradi na biashara nyingi ambazo zimekita mizizi humu xinjian. Baadhi ya miradi hii ndiyo tulizuru huku zoezi letu la ziara nchini China likishika mwendo. Kutoka Turpan tulifululiza hadi eneo la makavazi la Jiaohe. Eneo ambalo ni kumbu kumbu la maisha ya jadi kwa walioishi katika eneo hili karne zilizopita. Maeneo mawili ambayo siwezi kosa kuyataja ni kama vile mabaki ya makaburi za watoto mia mbili ambayo yametundikwa kwenye kijiji hicho. Haijulikani sababu ya vifo vya watoto hao lakini ni jambo ambalo hata kwa wanaoishi kando na makavazi hayo hawajapata kutatua.

Eneo lingine ni lile ambalo lina mabaki ya nyumba ambayo inadhaniwa kuwa la gavana wa kijiji hiki. Kulingana na vyombo vilivyopatikana humo jumba hiloLinaashiria kuwa kweli lilikuwa la mtu aliyekuwa kiongozi au wa umaarufu fulani. Vyombo vilivyopatikana ni kama vile umbo la ua la lotus na dragoni. Kutoka hapo tukaelekea hadi makavazi ya Karez eneo ambalo linatambulika kwa mifereji na vidimbwi iliyomo hadi futi mia moja chini ya ardhi. Mifereji hii nayo inatumiwa kunyunyuzia maji kwenye mashamba ya zabibu iliyomo kati ya mlima Tianchi na mji wa urumqi. Tianchi ni mlima ambao tulizuru jana na kugundua jinsi mbinu za kuhifadhi mazingira yanabuniwa na wakaazi wa Xinjiang. Ingawa mbinu za kuhifadhi mazingira zimebuniwa kwa wingi vidimbwi hivivyaendelea kukauka swala ambalo linatatiza jitihada za ukulima wa eneo la Turpan. Wakaazi wa Turpan kwa sasa wamejiingiza kwa biashara za utalii ili kujikimu kimaisha. Mwishowe tulizuru bonde linalotambulika kwa kukuza zainabu kando na milima mikuu. Eneo ambalo kwa sasa linaegemea kwa shughulii za utalii huku kilimo cha zainabu kikiwa msingi wa mila za wenyeji hapa. Hapo ndipo tunapotamatisha shughuli zetu kwa leo. Basi jiunge nami hapo kesho tutakapozuru eneo Yining kujua zaidi kuhusu maisha katika eneo hili.