Na Rashid Idi
Leo ilikuwa siku ya uzinduzi wa Xinjiang "through the lens",tulijumuika sote kusikiza hotoba fupi fupi ya naibu mkuu wa CRI Bi Wang na mkurugenzi wa habari Xinjiang Bi Hou. Wote walitueleza kwamba radio china kimataifa(cri)ni chombo muhimu cha habari kinacho fahamisha ulimwengu mambo ya China, na bila shaka maendeleo yote hapa mkoa wa Xinjiang. Bi Wang alihimiza kwamba vyombo vya habari havina budi kowapatanisha watu kote kwani vina uwezo wa kufanya hivyo.
Baada ya mkutano tulifunga safari kwenda kuzuru ziwa la tianchi,ilituchukuwa takribani lisaa moja hivi hadi tamati,mandhari hapa ni ya kuvutia mno, sote tuliwachwa na mshangao jinsi mazingira yalivyo kuwa ya kufana sana. Tuliasheriwa kwa makuli tamu mno kabla ya kuendelea na ziara zetu,naam,sina budi kukubaliana na msemo huu wa watu wa Uygur kuwa wageni wakija meza hujaa vyakula,kwa kweli xinjiang ina watu warimu mno. Ziarani tulikumbana na kina yahe wakiliwaza na uzuri wa Tianchi, lina vutio nzuri ya watalii,wenyenyeji na wageni wote walikuwa kwa harakati ya kuchukuwa picha hapa na pale ili kwa makumbusho yao,kwa wengeni ilikuwa ni wakati bora kwa kujivinjari na barafu zao za moyo.kwa kweli uhifadhi wa mazingira ina umuhimu sana kwa maisha yetu,haswa ziwa hili hapa huwasaidia sana watu wa mkoa huu kwa kilimo na uchumi,mwelekezi wetu wa kiswahili Han Mei alikuwa na ubora wa kutueleza manufaa haya.
Saa kumi na moja unusu hivi tukaanza safari ya kurudi zetu hotelini,macho yangu yakizidi kutazama niliko toka, Tianchi, "ziwa angani" moyoni nikiwaza kwamba nitarejea tena kwa majaliwa yake jalali kwani mchovya asali hachovyi mara moja……
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |