Siku ya tatu

cri 2011-09-18 12:16:30

Rashid

Mji mkongwe wa Jiaohe uko katika wilaya ya turpan karibu 200km mashariki mwa Urumqi. Inaaminika kwamba huu mji ni wa jadi mno, unarejelea miaka inarejelea miaka elfu moja iliyopita. Wakazi wamenufaika mno si haba kwa makavazi ya huu mji, umekuwa kivutio kikubwa cha utalii kwa wenyeji na wageni wa mbali.tulipo wasili hapa tulikumbana na foleni ya watu wa tabaka mbali mbali,wakongwe kwa vijana,wakubwa kwa wadogo,wote wakiwa na nia moja ya kujionea majenzi haya ya kale.makavazi haya yamekuwa uti wa uchumi kwa jamii hapa.

Tuliweza kutembelea pia ukuzaji wa zabibu,kilimo cha aina yake ambacho pia ni uti wa mgongo wa kiuchumi kwa jamii hapa,isitoshe mmea huu umerembesha mno na kufanywa paa ya biashara hapa kwani umeleta kivuli na urembesho wa kuvutia mno,mandhari haya pia huvutia wageni kwa wingi sana kama vile tulipojionea kweli wahenga hawakusea walipo nena kwamba akili ni mali,hii imedhihirishwa na jamii hii,yote tisa ya kumi ni miondoko ya kimadaha ya kitamaduni iliyotutumbuiza kwa mahanjamu yalioje....huna budi kuendelea kujiburudisha.

Tulizuru pia mifireji ya chini kwa chini ya kale, hii imenufaisha jamii kiuchumi kwani pia ni kivutio cha utalii,isitoshe kilimo kimeimarisha na huu mradi kwa wakati wa kiangazi kama vile Bi Han Mei mwelekezi wetu alitueleza. Xinjiang ni mkoa wa aina yake……