2: Siasa

Wajumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China

Xi Jinping

Alizaliwa mwezi Juni mwaka 1953 huko Fuping mkoani Shaanxi, China. Alianza kufanya kazi mwezi Januari mwaka 1969 na kujiunga na Chama cha Kikomunisti cha China mwezi Januari mwaka 1974. Alihitimu katika chuo cha utamaduni na jamii katika Chuo kikuu cha Qinghua, alipata digri ya uzamili na digri ya tatu ya sheria. Sasa ni Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya chama, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, na Mwenyekiti wa Kamati kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya Watu wa China.
Kuanzia mwaka 1969 hadi mwaka 1975 alikuwa katibu wa tawi la Chama cha Kikomunisti cha kitengo cha Liang Jiahe cha tarafa ya Wen'anyi huko Yanchuan mkoani Shaanxi.
Kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1979 alijifunza kozi ya kemikia sanisi ya kikaboni ya kimsingi katika kitivo cha kemikali cha Chuo kikuu cha Qinghua.
Kuanzia mwaka 1979 hadi mwaka 1982 alikuwa katibu wa ofisi ya baraza la serikali la China na Kamati kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya Watu wa China.
Kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1983 alikuwa naibu katibu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China huko Zhengding mkoani Hebei.
Kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1985 alikuwa katibu wa kamati ya kaunti, kamisaa wa siasa wa idara ya ulinzi, katibu wa kwanza wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China huko Zhengding mkoani Hebei.
Kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1988 alikuwa kamati ya kudumu ya kamati ya mji na naibu meya wa mji wa Xiamen mkoani Fujian
Kuanzia mwaka 1988 hadi mwaka 1990 alikuwa katibu wa kamati ya mji wa Ningde na katibu wa kwanza wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya eneo la kijeshi la mji huo.
Kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 1993 alikuwa katibu wa kamati ya mji wa Fuzhou, mkurugenzi wa kamati ya kudumu ya bunge la mji huo na katibu wa kwanza wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya eneo la kijeshi la mji huo.
Kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1995 alikuwa mjumbe wa kudumu wa kamati ya mkoa wa Fujian, katibu wa kamati ya mji wa Fuzhou, mkurugenzi wa kamati ya kudumu ya bunge la mji huo na katibu wa kwanza wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya eneo la kijeshi la mji huo.
Kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 1996 alikuwa naibu katibu wa kamati ya mkoa wa Fujian, katibu wa kamati ya mji wa Fuzhou, mkurugenzi wa kamati ya kudumu ya bunge la mji huo na katibu wa kwanza wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya eneo la kijeshi la mji huo.
Kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 1999 alikuwa naibu katibu wa kamati ya mkoa wa Fujian, kamisaa wa siasa wa idara ya akiba ya jeshi la mizinga mikubwa ya mkoa wa Fujian.
Kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000 alikuwa naibu katibu wa kamati ya mkoa wa Fujian, kaimu mkuu wa mkoa, naibu mkurugenzi wa kamati ya uhamasishaji wa ulinzi wa eneo la kijeshi la Nanjing, mkurugenzi wa kamati ya uhamasishaji wa ulinzi wa mkoa wa Fujian, kamisaa wa siasa wa idara ya akiba ya jeshi la mizinga mikubwa ya mkoa wa Fujian.
Kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000 alikuwa naibu katibu wa kamati ya mkoa wa Fujian, mkuu wa mkoa, naibu mkurugenzi wa kamati ya uhamasishaji wa ulinzi wa eneo la kijeshi la Nanjing, mkurugenzi wa kamati ya uhamasishaji wa ulinzi wa mkoa wa Fujian, kamisaa wa siasa wa idara ya akiba ya jeshi la mizinga mikubwa ya mkoa wa Fujian.
Kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2002 alijifunza kozi ya nadharia ya Umax na elimu ya fikra na siasa katika chuo cha utamaduni na jamii katika Chuo kikuu cha Qinghua, alipata digri ya tatu ya sheria.
Mwaka 2002 alikuwa naibu katibu wa kamati ya mkoa wa Zhejiang, kaimu mkuu wa mkoa, naibu mkurugenzi wa kamati ya uhamasishaji wa ulinzi wa eneo la kijeshi la Nanjing, mkurugenzi wa kamati ya uhamasishaji wa ulinzi wa mkoa wa Zhejiang.
Mwaka 2002 hadi mwaka 2003 alikuwa katibu wa kamati ya mkoa wa Zhejiang, kaimu mkuu wa mkoa, katibu wa kwanza wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya mkoa wa Zhejiang, naibu mkurugenzi wa kamati ya uhamasishaji wa ulinzi wa eneo la kijeshi la Nanjing, mkurugenzi wa kamati ya uhamasishaji wa ulinzi wa mkoa wa Zhejiang.
Mwaka 2003 hadi mwaka 2007 alikuwa katibu wa kamati ya mkoa wa Zhejiang, mkurugenzi wa kamati ya kudumu ya bunge la mkoa huo, na katibu wa kwanza wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya eneo la kijeshi la mkoa huo.
Mwaka 2007 alikuwa katibu wa mji wa Shanghai, katibu wa kwanza wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya eneo la ulinzi la mji huo.
Mwaka 2007 hadi mwaka 2008 alikuwa Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu, katibu wa sekretarieti ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, mkuu wa Chuo cha kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.
Mwaka 2008 hadi mwaka 2010 alikuwa Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu, katibu wa sekretarieti ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, mkuu wa Chuo cha kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.
Mwaka 2010 hadi mwaka 2012 alikuwa Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu, katibu wa sekretarieti ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Naibu Mwenyekiti wa Kamati kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya Watu wa China, mkuu wa Chuo cha kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.
Mwaka 2012 hadi mwaka 2013 alikuwa Katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya chama, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Watu wa China, na Naibu Mwenyekiti wa Kamati kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya Watu wa China
Mwaka 2013 hadi sasa amekuwa Katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya chama, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, na Mwenyekiti wa Kamati kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya Watu wa China.
Alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu ya 15, 16, 17, 18 na 19 za Chama cha Kikomunisti cha China, Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya 17, 18 na 19 ya chama. Alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China kwenye mkutano wa kwanza wa Bunge la umma la 11. Alichaguliwa kuwa Naibu mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya 17 ya Chama cha kikomunisti cha China, na kuchaguliwa kuwa Naibu mwenyekiti wa Kamati kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya watu wa China kwenye Mkutano wa Bunge la umma la 11. Kwenye Mkutano wa kwanza wa wajumbe wote wa Kamati kuu ya 18 ya chama, alichaguliwa kuwa Katibu mkuu wa Kamati kuu ya chama. Kwenye mkutano wa kwanza wa Bunge la umma la 12 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China na Mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya chama. Kwenye Mkutano wa kwanza wa wajumbe wote wa Kamati kuu ya 19 ya chama, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China

Li Keqiang

Alizaliwa mwezi Julai mwaka 1955 huko Dingyuan mkoani Anhui, China.  Alianza kufanya kazi mwezi Machi mwaka 1974, alijiunga na Chama cha Kikomunisti cha China mwezi Mei mwaka 1976. Alihitimu katika kitivo cha sheria na kitivo cha uchumi katika Chuo kikuu cha Beijing, alipata digri ya uzamili, digri ya kwanza ya sheria, na digri ya tatu ya uchumi.
Sasa ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, waziri mkuu, na katibu wa Kamati ya Chama.
Kuanzia mwaka 1974 hadi mwaka 1976 alifanya kazi ya kilimo katika kitengo cha DongLing cha tarafa ya Damiao huko Fengyang mkoani Anhui.
Kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1978 alikuwa katibu wa tawi la Chama cha Kikomunisti cha China la kitengo cha DongLing cha tarafa ya Damiao huko Fengyang mkoani Anhui.
Kuanzia mwaka 1978 hadi mwaka 1982 alijifunza katika kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Beijing.
Kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1983 alikuwa katibu wa kamati ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China katika Chuo Kikuu cha Beijing, na mjumbe wa kudumu wa Kamati kuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China.
Mwaka 1983 alikuwa mkuu wa idara ya shule ya Kamati kuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China na katibu mkuu wa shirika la wanafunzi la China.
Kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1985 alikuwa katibu mbadala wa Kamati kuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China.
Kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1993 alikuwa katibu wa Kamati kuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China na naibu mwenyekiti wa Shirika la Vijana la China.
Kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1998 alikuwa katibu wa kwanza wa Kamati kuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China na mkuu wa Chuo cha Elimu ya Siasa kwa Vijana cha China.
Kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 1999 alikuwa naibu katibu wa kamati ya mkoa wa Henan na kaimu mkuu wa mkoa.
Kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2002 alikuwa naibu katibu wa kamati ya mkoa wa Henan na mkuu wa mkoa.
Kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2003 alikuwa katibu wa kamati ya mkoa wa Henan na mkuu wa mkoa.
Kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2004 alikuwa katibu wa kamati ya mkoa wa Henan na mkurugenzi wa kamati ya kudumu ya bunge la mkoa huo.
Kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2005 alikuwa katibu wa kamati ya mkoa wa Liaoning.
Kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2007 alikuwa katibu wa kamati ya mkoa wa Liaoning na mkurugenzi wa kamati ya kudumu ya bunge la mkoa huo.
Kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2008 alikuwa Mjumbe wa kudumu wa Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China.
Kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2013 alikuwa Mjumbe wa kudumu wa Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China, Naibu waziri mkuu na Naibu katibu wa Kamati ya Chama.
Kuanzia mwaka 2013 hadi sasa amekuwa Mjumbe wa kudumu wa Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China, Waziri mkuu na Katibu wa Kamati ya Chama.
Alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu ya 15, 16, 17, 18 na 19 za Chama cha Kikomunisti cha China, Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya 17, 18 na 19 ya chama, na Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge la awamu ya 8 la China.

 

Li Zhanshu 

Bw. Li Zhanshu, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China, mkurugenzi wa Ofisi ya kamati ya usalama wa taifa ya Kamati kuu ya chama, na katibu wa kamati ya kazi ya ofisi zinazoongozwa moja kwa moja na Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China.
Alizaliwa mwezi wa Agosti, 1950 huko Pingshan mkoani Hebei. Alianza kazi mwezi Desemba, 1972 na kujiunga na Chama cha kikomunisti cha China mwezi Aprili, 1975. Bw. Li Zhanshu alihitimu kutoka kitivo cha ualimu wa siasa katika chuo kikuu cha ualimu cha Heibei, na alipata shahada ya pili ya usimamizi wa biashara.
Kuanzia mwaka 1971 hadi mwaka 1972 alisomea masomo kuhusu bei za bidhaa katika chuo cha mambo ya fedha na biashara cha eneo la Shijiazhuang, mkoani Hebei.
Kuanzia mwaka 1972 hadi mwaka 1976 alikuwa naibu mkurugenzi wa ofisi ya idara ya biashara ya eneo la Shijiazhuang mkoani Hebei.
Kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1983 alikuwa mkurugenzi wa kitengo cha makavazi cha Ofisi ya Kamati ya chama ya eneo la Shijiazhuang mkoani Hebei. Katika kipindi hicho, kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1983 alisoma katika kitivo cha ualimu wa kisiasa katika chuo kikuu cha ualimu cha Hebei wakati wa baada ya kazi.
Kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1985 alikuwa katibu wa kamati ya chama ya Wilaya ya Wuji ya mkoa wa Hebei.
Kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1986 alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama na mkurugenzi mkuu wa ofisi ya utawala ya eneo la Shijiazhuang mkoani Hebei .
Toka mwaka 1986 hadi 1990 alikuwa katibu wa kamati ya Jumuiya ya vijana ya Chama cha kikomunisti cha China ya mkoa wa Heibei, ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Agosti mwaka 1988, alishiriki kwenye semina ya mafunzo ya nadharia za ujenzi wa chama kwenye shule ya kamati kuu ya chama.
Kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 1993 alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama na mkurugenzi mkuu wa ofisi ya utawala ya eneo la Chengde mkoani Hebei.
Kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1997 alikuwa katibu mkuu na mjumbe wa kudumu wa kamati ya chama ya mkoa wa Hebei.
Kuanzia mwaka 1992 hadi mwaka 1994 alisomea masomo ya uchumi katika shule ya kamati kuu ya chama.
Kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 1998, alikuwa mjumbe wa kudumu wa kamati ya chama ya mkoa wa Hebei na naibu mkuu wa kikundi cha uongozi wa kazi za vijijini mkoani humo.
Kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2000, alikuwa mjumbe wa kudumu wa kamati ya chama ya mkoa wa Shaanxi, naibu mkuu wa kikundi cha uongozi wa kazi za vijijini na mkurugenzi wa ofisi ya kikundi hiki. Toka mwaka 1996 hadi mwaka 1998, alisomea shahada ya pili ya uchumi na biashara katika chuo cha Taasisi ya sayansi ya kijamii ya China.
Kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2002, alikuwa mjumbe wa kudumu wa kamati ya chama ya mkoa wa Shaanxi na mkurugenzi wa idara ya oganaizesheni ya kamati hiyo.
Mwaka 2002, alikuwa mjumbe wa kudumu wa kamati ya chama ya mkoa wa Shaanxi, katibu wa kamati ya chama ya mji wa Xi'an na mkurugenzi wa halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la mji huo.
Kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2003, alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama cha mkoa wa Shaanxi, katibu wa kamati ya chama ya mji wa Xi'an na mkurugenzi wa halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la mji huo.
Kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2004, alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama ya mkoa wa Heilongjiang.
Kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2007, alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama ya mkoa wa Heilongjiang na naibu mkuu wa mkoa huo. Katika kipindi hicho, kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2007, alisomea masomo ya usimamizi a ngazi ya juu wa viwanda na biashara katika chuo kikuu cha viwanda cha Harbin, na kupata shahada ya pili ya usimamizi wa ngazi ya juu wa viwanda na biashara.
Kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2008, alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama ya mkoa wa Heilongjiang, na kaimu mkuu wa mkoa huo.
Kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010, alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama ya mkoa wa Heilongjiang na mkuu wa mkoa huo.
Kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2012, alikuwa katibu wa kamati ya chama ya mkoa wa Guizhou, na mkurugenzi wa halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la mkoa huo.
Mwaka 2012, alikuwa naibu mkurugenzi wa Ofisi kuu ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, mkurugenzi wa ofisi hiyo, katibu wa kamati ya kazi ya ofisi zinazoongozwa moja kwa moja na kamati mkuu ya chama, na mkurugenzi wa halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la mkoa wa Guizhou.
Kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2014, alikuwa mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama, katibu wa ofisi ya sekretarieti ya kamati kuu ya chama, mkurugenzi wa ofisi kuu ya kamati kuu ya chama na katibu wa kamati ya kazi ya ofisi zinazoongozwa moja kwa moja na kamati kuu ya chama.
Kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2017, alikuwa mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, katibu wa ofisi ya sekretarieti ya kamati kuu ya chama, mkurugenzi wa ofisi kuu ya kamati kuu ya chama, mkurugenzi wa ofisi ya kamati ya usalama wa taifa ya Kamati kuu ya chama, na katibu wa kamati ya kazi ya ofisi zinazoongozwa moja kwa moja na kamati kuu ya chama.
Kuanzia mwaka 2017, amekuwa mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, mkurugenzi wa ofisi ya kamati ya usalama wa taifa ya kamati kuu ya chama, na katibu wa kamati ya kazi ya ofisi zinazoongozwa moja kwa moja na kamati kuu ya chama. Kabla ya hapo, alikuwa mjumbe mbadala wa kamati kuu ya 16 na 17 ya chama, mjumbe wa kamati kuu ya awamu za 18 na 19 ya chama, mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya 18 ya chama na katibu wa sekretarieti ya kamati kuu ya chama, na mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya 19 ya chama na mjumbe wa kudumu wa ofisi hiyo.

Wang Yang 

Bw. Wang Yang, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, naibu waziri mkuu na mjumbe wa ofisi ya chama katika baraza la serikali la China. Alizaliwa mwezi Machi mwaka 1955 katika mji wa Suzhou mkoani Anhui, alianza kazi mwezi Juni mwaka 1972, na kujiunga na Chama cha kikomunisti cha China mwezi Agosti mwaka 1975. Bw. Wang Yang alihitimu kutoka shule ya kamati kuu ya chama, na kupata shahada ya pili ya uhandisi.
Kuanzia mwaka 1972 hadi mwaka 1976, alikuwa mfanyakazi katika kiwanda cha vyakula cha eneo la Suxian mkoani Anhui, na mkurugenzi wa karakana ya kiwanda hicho.
Kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1979, alikuwa mwalimu wa shule ya makada wa chama ya eneo la Suxian mkoani Anhui, naibu mkurugenzi wa ofisi ya mafunzo na utafiti ya shule hiyo, na mjumbe wa kamati ya chama ya shule hiyo.
Kuanzia mwaka 1979 hadi mwaka 1980, alisomea masomo ya uchumi wa kisiasa kwenye semina ya mafunzo ya nadharia katika shule ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China.
Kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1981, alikuwa mwalimu katika shule ya kamati ya chama ya eneo la Suxian mkoani Anhui.
Kuanzia mwaka 1981 hadi mwaka 1982, alikuwa naibu katibu wa kamati ya Umoja wa vijana wa kikomunisti katika eneo la Suxian mkoani Anhui.
Kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1982, alikuwa mkurugenzi wa Ofisi ya uenezi ya Kamati ya Umoja wa vijana wa kikomunisti cha katika mkoa wa Anhui.
Kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1984, alikuwa naibu katibu wa Kamati ya Umoja wa vijana wa kikomunisti katika mkoa wa Anhui.
Kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, alikuwa naibu mkurugenzi wa kamati ya michezo ya mkoa wa Anhui, na naibu katibu wa Ofisi ya uongozi wa chama ya kamati hiyo.
Kuanzia mwaka 1987 hadi mwaka 1988, alikuwa mkurugenzi wa kamati ya michezo ya mkoa wa Anhui, na katibu wa Ofisi ya uongozi wa chama ya kamati hiyo. Kuanzia mwaka 1988 hadi mwaka 1992, alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama ya mji wa Tongling wa mkoa wa Anhui, kaimu meya na meya wa mji huo. Katika kipindi hicho kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 1992, alisomea masomo ya shahada ya kwanza ya usimamizi wa mambo ya utawala ya chama na serikali katika shule ya kamati kuu ya chama.
Kuanzia mwaka 1992 hadi mwaka 1993, alikuwa mkurugenzi wa kamati ya mipango ya mkoa wa Anhui, katibu wa Ofisi ya uongozi wa chama ya kamati hiyo na msaidizi wa mkuu wa mkoa wa Anhui.
Mwaka 1993 alikuwa naibu mkuu wa mkoa wa Anhui.
Kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1998, alikuwa mjumbe wa kudumu wa kamati ya chama ya mkoa wa Anhui na naibu mkuu wa mkoa huo. Katika kipindi hicho, kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1995 alisomea masomo ya menejimenti kwenye kitivo cha sayansi ya usimamizi katika Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha China na kupata shahada ya pili; kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei mwaka 1997, alishiriki kwenye semina ya mafunzo kwa maofisa waandamizi wa mikoa katika shule ya kamati kuu ya chama.
Kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 1999, alikuwa naibu katibu wa kamati ya chama ya mkoa wa Anhui, na naibu mkuu wa mkoa huo.
Kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2003, alikuwa naibu mkurugenzi wa kamati ya taifa ya maendeleo na mipango, na mjumbe wa Ofisi ya uongozi wa chama katika kamati hiyo. Katika kipindi hicho kuanzia mwezi Septemba hadi Novemba mwaka 2001, alishiriki kwenye semina ya mafunzo kwa maofisa waandamizi wa mikoa katika shule ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China.
Kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2005, alikuwa naibu katibu mkuu wa Baraza la serikali la China, anayesimamia kazi za Ofisi kuu na naibu katibu wa Ofisi ya uongozi wa chama katika baraza la serikali la China.
Kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2006, alikuwa katibu wa kamati ya chama ya mji wa Chongqing.
Kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2007, alikuwa katibu wa kamati ya chama ya mji wa Chongqing, na mkurugenzi wa halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la mji wa Chongqing.
Mwaka 2007 alikuwa mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, katibu wa kamati ya chama ya mji wa Chongqing na mkurugenzi wa halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la mji wa Chongqing.
Kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2012, alikuwa mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama, na katibu wa kamati ya chama ya mkoa wa Guangdong.
Kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2013, alikuwa mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China.
Kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2017, alikuwa mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama, naibu waziri mkuu na mjumbe wa Ofisi ya uongozi wa chama katika Baraza la serikali la China.
Mwaka 2017, amekuwa mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, naibu waziri mkuu na mjumbe wa Ofisi ya uongozi wa chama katika baraza la serikali la China.
Pia aliwahi kuwa mjumbe mbadala wa kamati kuu ya 16 ya chama cha kikomunisti cha China, mjumbe wa kamati kuu ya 17, ya 18 na ya 19 ya chama, mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya 17 na ya 18 za chama, na mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya 19 ya chama na mjumbe wa kudumu wa ofisi hiyo.

 

Wang Huning 

 Bw. Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC, ambaye pia ni katibu wa ofisi ya Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati Kuu ya CPC, na mkurugenzi wa Ofisi ya Kikundi cha Uongozi wa kuendeleza kwa kina Mageuzi  ya Kamati Kuu ya CPC. 
 Alizaliwa mwezi Oktoba,1955 katika wilaya ya Laizhou, mkoani Shandong. Alianza kufanya kazi mwezi Februari, mwaka 1977, na kujiunga na Chama cha Kikomunisti cha China CPC mwezi Aprili, 1984. Alihitimu masomo ya kozi ya siasa ya kimataifa ya shahada ya pili katika Kitivo cha siasa ya kimataifa cha Chuo Kikuu cha Fudan, na pia alipata shahada ya pili ya kozi ya sheria. Alikuwa profesa wa Chuo Kikuu cha Fudan. 
 Mwaka 1972 hadi 1977, alisoma katika semina ya lugha za kigeni iliyoandaliwa na chuo cha maofisa cha Chuo kikuu cha Ualimu cha Shanghai.
 Mwaka 1977 hadi 1978, alifanya kazi katika Shirika la Uchapishaji la Shanghai.
 Mwaka 1981 hadi 1989, alikuwa mwalimu, naibu profesa na profesa wa kitivo cha siasa ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Fudan.
 Mwaka 1989 hadi 1994, alikuwa mkurugenzi wa Ofisi ya siasa ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Fudan.
 Mwaka 1994 hadi 1995, alikuwa mkurugenzi wa chuo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Fudan.
 Mwaka 1995 hadi 1998, alikuwa mkuu wa kikundi cha siasa cha Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati kuu ya CPC.
 Mwaka 1998 hadi 2002, alikuwa naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati kuu ya CPC.
 Mwaka 2002 hadi 2007, alikuwa mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati kuu ya CPC.
 Mwaka 2007 hadi 2012, alikuwa katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, na mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati Kuu ya CPC.
 Mwaka 2012 hadi 2014, alikuwa mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, na mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati Kuu ya CPC.
 Mwaka 2014 hadi 2017, alikuwa mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati Kuu ya CPC, na mkurugenzi wa Ofisi ya Kikundi cha Uongozi wa Kukuza Mageuzi kwa Pande Zote ya Kamati Kuu ya CPC.
 Mwaka 2017 hadi sasa, yeye ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, katibu wa Ofisi ya Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati Kuu ya CPC, na mkurugenzi wa Ofisi ya Kikundi cha Uongozi wa Kuendeleza kwa kina Mageuzi ya Kamati Kuu ya CPC.
 Alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya awamu ya 16,17 na 18 ya CPC, katibu wa Ofisi ya Sekretarieti ya Kamati Kuu ya 17 ya CPC, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya 18 ya CPC, na mjumbe, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa, katibu wa ofisi ya Sekretarieti ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC.

Zhao Leji 

 Bw. Zhao Leji, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, katibu wa Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Kamati Kuu ya CPC, na mkuu wa Ofisi inayoshughulikia nguvukazi na ujenzi wa chama ya Kamati Kuu ya CPC.
 Yeye alizaliwa mwezi Machi, 1957 mjini Xian, mkoani Shaanxi. Alianza kufanya kazi mwezi Septemba, mwaka 1974, na kujiunga na Chama cha CPC mwezi Julai mwaka 1975. Alihitimu masomo ya shahada ya pili katika Chuo cha Kamati Kuu ya CPC. 
  Mwaka 1974 hadi 1975, alifanya kazi ya kilimo katika kitengo cha Gongba cha tarafa ya Hedong ya wilaya ya Guide, mkoani Qinghai.
 Mwaka 1975 hadi 1977, alifanya kazi ya kupeleka nyaraka katika idara ya biashara ya serikali ya mkoa wa Qinghai.
 Mwaka 1977 hadi 1980, alisoma kozi ya falsafa katika Kitivo cha falsafa ya Chuo Kikuu cha Beijing.
 Mwaka 1980 hadi 1982, alikuwa ofisa wa Ofisi ya siasa ya Idara ya biashara ya serikali ya Mkoa wa Qinghai, mwalimu na katibu wa Umoja wa vijana wa Kikomunisti katika Chuo cha Biashara ya mkoa wa Qinghai.
 Mwaka 1982 hadi 1983, alikuwa naibu mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya mafundisho ya Chuo cha Biashara ya mkoa wa Qinghai.
 Mwaka 1983 hadi 1984, alikuwa naibu mkurugenzi wa ofisi ya siasa katika Idara ya biashara ya serikali ya mkoa wa Qinghai, na katibu wa Umoja wa vijana wa kikomunisti wa idara hiyo.
 Mwaka 1984 hadi 1986, alikuwa meneja na katibu wa kamati ya CPC katika Kampuni ya Vifaa vya Metali na Umeme, na Shughuli za Kemikali ya mkoa wa Qinghai.
 Mwaka 1986 hadi 1991, alikuwa naibu mkuu wa idara ya biashara ya serikali ya mkoa wa Qinghai, na naibu katibu wa kamati ya CPC ya idara hiyo. 
 Mwaka 1991 hadi 1993, alikuwa mkuu wa idara ya biashara ya serikali ya mkoa wa Qinghai, na katibu wa kamati kuu ya CPC ya idara hiyo( pia alikuwa mkurugenzi wa Shirikisho la Mauzo na Manunuzi la mkoa wa Qinghai mwezi Aprili mwaka 1992).
 Mwaka 1993 hadi 1994, alikuwa msaidizi wa mkuu wa mkoa wa Qinghai, mkuu wa idara ya fedha ya serikali ya mkoa wa Qinghai, na katibu wa kamati ya CPC ya idara hiyo.
 Mwaka 1994 hadi 1995, alikuwa naibu mkuu wa mkoa wa Qinghai, mkuu wa idara ya fedha ya serikali ya mkoa wa Qinghai, na katibu wa kamati ya CPC ya idara hiyo.
 Mwaka 1995 hadi 1997, alikuwa naibu mkuu wa mkoa wa Qinghai.
 Mwaka 1997 hadi 1997, alikuwa naibu mkuu wa mkoa wa Qinghai, na katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Xining, mkoani Qinghai.
 Mwaka 1997 hadi 1999, alikuwa naibu mkuu wa mkoa wa Qinghai, na katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Xining, mkoani Qinghai.
 Mwaka 1999 hadi 2000, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mkoa wa Qinghai, na kaimu mkuu wa mkoa huo.
 Mwaka 2000 hadi 2003, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mkoa wa Qinghai, na mkuu wa mkoa huo.
 Mwaka 2003 hadi 2003, alikuwa katibu wa kamati ya CPC ya mkoa wa Qinghai, na mkuu wa mkoa huo.
 Mwaka 2003 hadi 2004, alikuwa katibu wa kamati ya CPC ya mkoa wa Qinghai.
 Mwaka 2004 hadi 2007, alikuwa katibu wa kamati ya CPC ya mkoa wa Qinghai, na mkurugenzi wa Baraza la Kudumu la Bunge la Umma la mkoa huo.
 Mwaka 2007 hadi 2008, alikuwa katibu wa kamati ya CPC ya mkoa wa Shaanxi.
 Mwaka 2008 hadi 2012, alikuwa katibu wa kamati ya CPC ya mkoa wa Shaanxi, na mkurugenzi wa Baraza la Kudumu la Bunge la Umma la mkoa huo.
 Mwaka 2012 hadi 2017, alikuwa mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, katibu wa Ofisi ya Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, na mkuu wa Ofisi inayoshughulikia nguvukazi na ujenzi wa chama ya Kamati Kuu ya CPC.
 Alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya awamu ya 16,17 na 19 ya CPC, mjumbe wa Ofisi ya Siasa na katibu wa ofisi ya Sekretarieti ya Kamati kuu ya 18 ya CPC, mjumbe na mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC, na mjumbe, mjumbe wa kudumu na katiba ya Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC.

Han Zheng

 Bw. Han Zheng, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC alizaliwa mwezi Aprili, 1954 katika wilaya ya Cixi mkoani Zhejiang. Alianza kufanya kazi mwezi Desemba, 1975, na kujiunga na Chama cha Kikomunisti cha China CPC mwezi Aprili, 1979. Alihitimu masomo ya kozi ya uhusiano wa kimataifa na uchumi wa dunia katika taasisi ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Huadong, na pia alipata shahada ya pili ya kozi ya uchumi. Alikuwa mtaalamu wa ngazi ya juu wa uchumi. 
 Mwaka 1975 hadi 1980, alikuwa msimamizi wa ghala, mfanyakazi wa ofisi ya mauzo na manunuzi, na naibu katibu wa Umoja wa vijana wa kikomunisti katika Shirika la Unyanyuaji na Ufungaji wa Vitu Vizito la Xuhui la Shanghai.
 Mwaka 1980 hadi 1982, alikuwa mfanyakazi na mkuu wa Umoja wa vijana wa kikomunisti wa Kampuni ya Vifaa vya Shughuli za Kemikali ya Shanghai.
 Mwaka 1982 hadi 1986, alikuwa katibu wa Umoja wa vijana wa kikomunisti wa Idara ya viwanda vya kemikali ya Shanghai.
 Mwaka 1986 hadi 1987, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya Chuo cha Viwanda vya kemikali cha Shanghai.
 Mwaka 1987 hadi 1988, alikuwa katibu wa kamati ya CPC na naibu mkuu wa Kiwanda cha Viatu vya Raba cha Shanghai.
 Mwaka 1988 hadi 1990, alikuwa katibu wa kamati ya CPC na naibu mkuu wa Kiwanda cha Mipira cha taifa cha Shanghai.
 Mwaka 1990 hadi 1991, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya Umoja wa vijana wa kikomunisti wa Shanghai.
 Mwaka 1991 hadi 1992, alikuwa katibu wa kamati ya CPC ya Umoja wa vijana wa kikomunisti wa Shanghai.
 Mwaka 1992 hadi 1993, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC na kaimu mkuu wa eneo la Luwan la mji wa Shanghai.
 Mwaka 1993 hadi 1995, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC na mkuu wa eneo la Luwan la Shanghai.
 Mwaka 1995 hadi 1997, alikuwa naibu katibu mkuu wa serikali ya mji wa Shanghai, naibu katibu wa kamati ya CPC inayoshughulikia kazi za uchumi wa mji wa Shanghai, mkurugenzi na katibu wa tume ya CPC wa kamati ya uzazi kwa mpango ya mji wa Shanghai, na mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa hila ya serikali ya mji wa Shanghai.
 Mwaka 1997 hadi 1998, alikuwa mjumbe wa kudumu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, na naibu katibu mkuu wa serikali ya mji wa Shanghai.
 Mwaka 1998 hadi 2002, alikuwa mjumbe wa kudumu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, na naibu mkuu wa mji wa Shanghai.
 Mwaka 2002 hadi 2003, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, na naibu meya wa mji wa Shanghai.
 Mwaka 2003 hadi 2004, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, na meya wa mji wa Shanghai.
 Mwaka 2004 hadi 2006, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, meya wa mji wa Shanghai, naibu mkurugenzi wa Tume ya maandalizi na mkurugenzi mtendaji wa Tume ya utendaji ya Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010.
 Mwaka 2006 hadi 2007, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, meya wa mji wa Shanghai,naibu mkurugenzi wa Tume ya maandalizi, naibu mkurugenzi wa kwanza, mkurugenzi mtendaji na mkurugenzi wa tume ya utendaji ya Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010.
 Mwaka 2007 hadi 2008, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, meya wa mji wa Shanghai, naibu mkurugenzi wa kwanza, mkurugenzi wa Tume ya utendaji ya Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010.
 Mwaka 2008 hadi 2011, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, meya wa mji wa Shanghai,naibu mkurugenzi wa Tume ya maandalizi, mkurugenzi mtendaji wa Tume ya utendaji ya Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010.
 Mwaka 2011 hadi 2012, alikuwa naibu katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai, na meya wa mji wa Shanghai.
 Mwaka 2012 hadi 2017, alikuwa mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, na katibu wa kamati ya CPC ya mji wa Shanghai.
 Alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya awamu ya 16,17,na 18 ya CPC, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya 18 ya CPC, mjumbe na mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC.

 


1  2  3  4  5