9: Hifadhi ya Mazingira

Mashirika na jumuiya za hifadhi ya mazingira

Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya taifa Radio China Kimataifa

Mwaka 1998, kutokana na uthibitishaji wa mkutano wa kwanza wa Bunge la 9 la umma la China na mpango husika wa Baraza la serikali la China kuhusu mageuzi ya mashirika, China iliweka rasmi Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya taifa (ngazi yake inalingana na wizara). Jukumu lake kuu ni kutunga sera na sheria za hifadhi ya mazingira ya nchi, kutunga kanuni za utawala, kusimamia shughuli za uendelezaji na matumizi ya maliasili katika sehemu za maumbile zinazoweza kuleta athari mbaya kwa hifadhi ya mazingira ya viumbe, ujenzi wa miradi muhimu ya mazingira ya viumbe na kazi ya kufufua hali ya uharibifu kwa mazingira ya viumbe na kadhalika. Idara hiyo kuu pia ina idara zake kwenye ngazi mbalimbali. Na mkuu wa hivi sasa wa Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya taifa ya China ni Bwana Xie Zhenhua.

Anuani ya tovuti ya idara hiyo ni: http://www.zhb.gov.cn

Kamati ya ushirikiano wa kimataifa wa mazingira na maendeleo ya China

Mwaka 1992, serikali ya China iliidhinisha Kamati ya ushirikiano wa kimataifa wa mazingira na maendeleo ya China. Kamati hiyo ni idara ya utoaji ushauri ya kimataifa ya ngazi ya juu, wadhifa wa mwenyekiti wake huchukuliwa na mawaziri au manaibu mawaziri wa baraza la serikali la Jamhuri ya watu wa China (mwenyekiti wake wa sasa ni naibu waziri mkuu Bwana Zeng Peiyan). Jukumu lake kuu ni kutoa mapendekezo ya kisera kuhusu masuala makubwa, muhimu na ya dharura yanayohusu sekta za mazingira na maendeleo ya China, pia kutoa vielelezo vya kisera na kimradi. Kamati hiyo inaundwa na mawaziri au manaibu mawaziri, wataalamu mashuhuri wa sekta ya mazingira na maendeleo, maprofesa pamoja na mawaziri wa nchi nyingine na viongozi wa jumuia za kimataifa.

Anuani ya tovuti ya kamati hiyo kwenye mtandao wa Iternet ni: http://www.cciced.org

Mfuko wa hifadhi ya mazingira ya China

Mfuko huo ulianzishwa mwezi Aprili mwaka 1993, ambao ni shirikisho la jamii lisilotafuta faida na lenye haki ya kuwa mwakilishi wa kisheria, nao ni mfuko wa kwanza wa kiraia wa China unaoshughulikia shughuli za hifadhi ya mazingira. Mfuko huo unafuata kanuni ya "kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi, kuzitumia fedha hizo kwa kuwahudumia wananchi na kuleta heri na baraka kwa binadamu", ukichangisha fedha kwa njia mbalimbali, na kuzitumia kwa kuwatunukia mashirika au watu waliotoa mchango mkubwa kwa kuhifadhi mazingira ya China, kusaidia shughuli na miradi ya aina mbalimbali inayohusika na hifadhi ya mazingira, kuanzisha maingiliano na ushirikiano wa kiteknolojia na nchi za nje katika sekta ya hifadhi ya mazingira, kusukuma mbele maendeleo ya kazi mbalimbali za hifadhi ya mazingira kama vile usimamizi wa hifadhi ya mazingira ya China, utafiti wake wa kisayansi, uenezi na utoaji elimu, kuwaandaa wataalamu wa hifadhi ya mazingira, kufanya maingiliano ya kitaaluma, kuendeleza shughuli za hifadhi ya mazingira na shughuli mbalimbali zinazohusiana na nchi za nje.

Anuani ya tuvuti ya Mfuko wa hifadhi ya mazingira ya China (CEPF) kwenye mtandao wa internet ni : http://www.cepf.org.cn/

Shirikisho la Marafiki wa dunia ya maumbile

Tawi la utamaduni wa dunia ya maumbile la Chuo cha utamaduni wa China (kwa kawaida linaitwa "Shirikisho la marafiki wa dunia ya maumbile") ni kundi la kwanza la kiraia la hifadhi ya mazingira lililoidhinishwa na serikali ya China mwezi Machi mwaka 1994. Mwazilishi wake na mkuu wake wa sasa ni Profesa Liang Congjie. Shirikisho hilo linafuata nia ya kuanzisha elimu ya kiumma ya hifadhi ya mazingira, kutetea ustaarabu wa hifadhi ya mazingira ya kimaumbile, kutetea na kueneza utamaduni wenye umaalumu wa kichina kuhusu hifadhi ya mazingira na kusukuma mbele maendeleo ya hifadhi ya maumbile ya China.

Tovuti ya shirikisho hilo kwenye mtandao wa internet ni: http://www.fon.org.cn/

Shirikisho la hifadhi ya mazingira ya kimaumbile ya Beijing

Shirikisho hilo ni shirikisho la watu wa kujitolea wa hifadhi ya mazingira lililoanzishwa kwenye mtandao wa internet, shirikisho hilo linatekeleza kabisa utaratibu wa watu wa kujitolea wafanye juhudi za kuhifadhi mazingira, ili kuwahamasisha raia wote washiriki katika shughuli za hifadhi ya mazingira ya China. Shirikisho hilo ni kundi la vijana wanaojitolea wenye ukakamavu na ari kubwa, liliwahi kuanzisha harakati za kuwaokoa "swala la Tibet".

Anuani ya tovuti ya shirikisho hilo kwenye mtandao wa internet ni : http://gbj.grchina.net/

Mshirikisho mengine ya kiserikali ya hifadhi ya mazingira ya China

Tovuti ya uokoaji wa maliasili na hifadhi ya mazingira ya China: http://www.drccu.gov.cn Idara ya hifadhi ya mazingira ya Beijing: http://www.bjepb.gov.cn/ Mazingira ya Shanghai: http://www.sepb.gov.cn/ Hifadhi ya mazingira ya Guangdong: http://www.gdepb.gov.cn/ Hifadhi ya mazingira ya Fujian: http://fjepb.fj.cn.net/ Hifadhi ya mazingira ya Xinjiang: http://www.xjepb.gov.cn/ Tovuti ya Upashanaji habari wa hifadhi ya mazingira ya Liaoning: http://www.lnepb.gov.cn/ Hifadhi ya mazingira ya Anhui: http://www.aepb.gov.cn/ Maendeleo endelevu ya Mkoa wa Anhui: http://www.anhuisd.com/ Hifadhi ya mazingira ya Shenyang: http://www.syepe.com Taasisi ya utafiti wa sayansi ya hifadhi ya mazingira ya Chengdu: http://cdhbkys.ep.net.cn/ Maendeleo endelevu ya Shenyang: http://www.sdos.org/

Mashirikisho mengine ya hifadhi ya mazingira yasioyo ya kiserikali ya China(NGO)

Taasisi ya utafiti wa mazingira na maendeleo: http://www.ied.org.cn/ Kijiji cha dunia cha Beijing: http://www.gvbchina.org/chinese.htm Marafiki wa dunia (Hong Kong):http://www.foe.org.hk/ Taasisi ya utafiti wa maendeleo endelevu ya China: http://cssd.acca21.org.cn/99plan.html Watu wanaojotolea wa maskani ya kimaumbile:http://www.greenearth.hypermart.net/


1 2 3 4 5 6