Ardhi ya taifa

中国国际广播电台


     
Eneo la ardhi

Jamhuri ya Watu wa China yaani China, iko kwenye sehemu ya mashariki ya Bara la Asia na kando ya magharibi ya Bahari ya Pasifiki. Eneo la nchi kavu la China ni karibu kilomita za mraba milioni 9.6, ambayo ni nchi yenye eneo kubwa zaidi kwenye Bara la Asia, na ni nchi kubwa ya tatu duniani ikizifuata Russia na Canada.

Toka kaskazini hadi kusini, ardhi ya China inaanzia kwenye chanzo cha Mto Heilongjiang, kaskazini ya Mto Mo (digri 53.30 ya latitudo ya kaskazini) mpaka Zengmu Ansha ya ncha ya kusini ya Visiwa vya Nasha (digrii 4 ya latitude ya kaskazini), umbali kati ya kusini na kaskazini ni kilomita 5500; toka mashariki hadi magharibi, ardhi ya China inaanzia sehemu ya makutano kati ya Mto Heilong na Mto Usuri (digrii 135.05 ya longitudo ya mashariki), mpaka Uwanda wa juu wa Pamier (digri ya 73.40 ya longitude), umbali kati ya mashariki na magharibi ni kilomita 5000.

Mpaka wa nchi kavu ya China una urefu wa kilomita 22,800, upande wa mashariki, China inapakana na Korea ya kaskazini, upande wa kaskazini inapakana na Mongolia, upande wa mashariki inapakana na Russia, upande wa kaskazini magharibi inapakana na Kazakstan, Kyrgyzstan na Tajikstan, upande wa magharibi na wa kusini magharibi inapakana na Afgahnistan, Pakistan, India, Nepal, na Buthan, upande wa kusini inapakana na Myanmar, Laos na Vietnam. Na upande wa mashariki na wa kusini mashariki China inakabiliana kwa bahari na Korea ya kusini, Japan, Philipines, Burnei, Malaysia na Indonesia.