中国国际广播电台
Bendera ya Taifa
Bendera
ya Taifa, Nembo la Taifa,
Wimbo la Taifa na Mji Mkuu
Bendera ya Taifa: Bendera
ya Taifa la Jamhuri ya Watu
wa China ni Bendera nyekundu
yenye nyota tano za manjano,
kiasi cha ulinganifu kati
ya urefu na kimo cha bedera
hiyo ni 3:2. Bendera ya Taifa
ina rangi nyekundu ambayo
inamaanisha mapinduzi. Nyota
5 zenye pembe 5 kwenye bendera
hiyo ni za rangi ya manjano,
na kila ncha ya nyota 4 ndogo
zenye pembe 5 inaielekea katikakati
ya nyota kubwa, ambayo inaonesha
mshikamano mkubwa wa wananchi
chini ya uongozi wa Chama
cha kikomunisti cha China.
Nembo ya Taifa
ya Jamhuri ya Watu wa China
Nembo ya Taifa ya Jamhuri
ya Watu wa China: Nembo ya
Taifa ya Jamhuri ya Watu wa
China inaonesha Bendera ya
Taifa, Uwanja wa Tian An Men,
gurudumu lenye meno na mashuke
ya ngano na mpunga, ambayo
inamaanisha mapambano ya mapinduzi
ya demokrasia mpya yaliyofanyika
tokea harakati za “tarehe
4 Mei” mwaka 1919 na wananchi
wa China pamoja na kuzaliwa
kwa China mpya yenye utawala
wa kidemokrkasi wa uumma chini
ya uongozi wa tabaka la wafayakazi
na kwenye msingi wa shirikisho
la wafanyakazi na wakulima.
Wimbo wa Taifa
Wimbo wa Taifa wa Jamhuri
ya Watu wa China ni wimbo
wa “Songa mbele watu mliojitolea”,
ambao ulitungwa mwaka 1935,
mtungaji wa maneno ya wimbo
huu ni mwandishi maarufu wa
tamthiria Bwana Tian Han,
muziki wa wimbo huu ulitungwa
na Bwana Nie Er ambaye alikuwa
mwanzilishi wa harakati za
muziki mpya wa China. Wimbo
huo ulikuwa wimbo wa kauli
mbiu ya filamu ya “Vijana
waliokumbwa na mashambulizi”.
Filamu hiyo ilieleza kuwa
baada ya tukio la “Tarehe
18 Septemba” mwaka 1931, Japan
iliposhambulia na kuikalia
mikoa mitatu ya kaskazini
mashariki ya China, taifa
la China lilikuwa katika kipindi
cha kufa na kupona, ambapo
baadhi ya vijana walijitoa
kutoka kwenye hali ya uchungu
na mahangaiko wakaenda kwenye
medani ya vita kupambana na
mashambulizi ya Japan. Kutokana
na filamu hiyo, wimbo huu
uliimbwa na wachina wa kila
sehemu nchini China, ukasifiwa
kuwa mbiu wa kutoa mwito wa
kujipatia ukombozi wa taifa
la China.
Tarehe 27 Septemba mwaka 1949,
mkutano wa kwanza wa wajumbe
wote wa Baraza la mashauriano
ya kisiasa la umma la China
ulipitisha azimio kuwa kabla
ya kutungwa rasmi kwa wimbo
wa taifa wa Jamhuri ya Watu
wa China, wimbo wa “Songa
mbele watu mliojitolea” uwe
wimbo wa taifa. Tarehe 14
Machi, mwaka 2004, Mkutano
wa pili wa Halmashauri ya
kudumu ya 10 ya Bunge la umma
la China ulipitisha mswada
wa marekebisho ya katiba ukaamua
kuwa wimbo wa Taifa wa Jamhuri
ya Watu wa China ni wimbo
wa “Songa mbele watu mliojitolea
”.
Wimbo wa Taifa
Nyanyukeni!
Enyi msiokubali kuwa watumwa!
Tujenge ukuta mkuu mpya kwa damu na miili yetu!
Taifa la China limekuwa hatarini kabisa,
Kila mmoja analazimika kupaaza sauti ya mwisho.
Nyanyukeni, nyanyukeni, nyanyukeni!
Sote tuwe na nia moja,
Tusonge mbele bila kujali risasi na mizinga!
Tusonge mbele bila kujali risasi na mizinga!
Mbele! mbele! mbele!
Mji Mkuu wa
Jamhuri ya Watu wa China
Mji mkuu wa Jamhuri ya Watu
wa China ni Beijing.
Tarehe mosi Oktoba mwaka 1949 mwenyekiti Mao Zedong kwenye roshani ya Tian An Men alitangaza dunia nzima kuwa serikali kuu ya Jamhuri ya Watu wa China imeasisiwa! Tokea hapo, Beijing ukiwa mji mkuu pamoja na China mpya umefungua ukurasa mpya wa historia.
|