中国国际广播电台
Mwambao wa nchi kavu ya China
unaanzia mlango wa Mto Yalu
wa Mkoa wa Liaoning wa kaskazini
hadi Mlango wa Mto Beilun
wa Mkoa wa Guangxi wa kusini,
urefu wake ni kilomita 1,800.
Hali ya kijiografia ya pwani
za bahari ni tambarare, ambapo
kuna bandari na ghuba nyingi
zenye hali bora, na nyingi
ni bandari ambazo maji yake
hayawezi kuganda kwa mwaka
mzima. Kuna bahari kubwa 5
za karibu nchini China kama
vile Bahari ya Bo, Bahari
ya Huang, Bahari ya Mashariki,
Bahari ya Kusini pamoja na
Sehemu ya Bahari ya Pasifiki
ya mashariki ya Taiwan. Miongoni
mwa hizo, Bahari ya Bo ni
bahari ya ndani ya China.
Sehemu ya Bahari ya Pasifiki
ya mashariki ya Taiwan inaanzia
Visiwa vya Xiandao vya kaskazini
vilivyoko kusini magharibi
ya Visiwa vya Ryukyu vya Japan,
mpaka kwenye Mlango wa Bahari
ya Bashi wa kusini.
Eneo la bahari la China ni
pamoja na maji ya ndani na
mamlaka ya bahari ya China,
eneo lake la jumla ni zaidi
ya kilomita 380,000. Maji
ya ndani ya China ni eneo
la bahari la Jamhuri ya watu
wa China toka mstari wa mamlaka
ya bahari unaoelekea upande
wa nchi kavu hadi mwambao
wa bahari. Upana wa mamlaka
ya bahari ya China ni nautical
maili 12 kuanzia mstari wa
bahari.
Kwenye eneo la bahari ya
China kuna visiwa zaidi ya
5000, eneo lake la jumla ni
kilomita za mraba 80,000,
mwambao wa visiwa ni kilomita
za mraba 14,000. Miongoni
mwao Kisiwa cha Taiwan ni
kikubwa zaidi kuliko vingine
vyote, eneo lake ni kilomita
za mraba 36,000; Kisiwa cha
Hainan ni cha pili kwa ukubwa
wake, eneo lake ni kilomita
za mraba 34,000. Visiwa vya
Diaoyu na Visiwa vya Chiwei
vilivyoko kwenye bahari ya
kaskazini mashariki ya Kisiwa
cha Taiwan ni visiwa vilivyoko
kwenye sehemu ya mashariki
kabisa ya China. Visiwa vya
Dongsha, Visiwa vya Xisha,
Visiwa vya Zhongshan na Visiwa
vya Nasha vilivyoko kusini
kabisa ya China vinaitwa kuwa
ni visiwa mbalimbali vya Bahari
ya Kusini.
|