中国国际广播电台
Hali ya JiografiaChina ni nchi yenye milima
mingi, eneo la sehemu za milimani
linachukua theluthi mbili
ya eneo la jumla la nchi nzima.
Sehemu hizo za milimani ni
pamoja na ardhi milimani,
vilima na nyanda za juu. Katika
eneo lote la China ardhi ya
milima inachukua 33 %, nyanda
za juu 26 %, mabonde 19 %,
tambarare 12 % na vilima 10
%.
Katika mamilioni ya miaka
kadhaa iliyopita, Uwanda wa
Juu wa Qinghai-Tibet ulikuwa
kama nundu kwenye ardhi duniani,
maumbo ya ardhi ya China yakatokana
na uwanda huo. Ukiiangalia
ardhi ya China kutoka angani,
hali ya kijiografia ya China
ni kama ngazi inayoelekea
mashariki kutoka magharibi,
inatelemka hatua kwa hatua.
Kutokana na kugongana kati
ya ardhi ya India na ardhi
ya Ulaya na Asia, Uwanda wa
Juu wa Qinghai-Tibet ulijitokeza
siku hadi siku, mwinuko wake
kwenye usawa wa bahari ni
zaidi ya mita 4000, hivyo
uwanda huo unaitwa kuwa ni
“Paa la dunia”, na kuwa ngazi
ya kwanza kwenye ardhi ya
China. Kilele kikuu cha Jomolangma
cha Mlima Himalaya kwenye
Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet
kina urefu wa mita 8848.13,
ambacho ni kilele cha juu
cha kwanza duniani. Ngazi
ya pili inaundwa na Uwanda
wa Juu wa Mongolia ya ndani,
Uwanda wa juu wa Huangtu,
Uwanda wa Juu wa Yungui pamoja
na Bonde la Talimu, Bonde
la Zhungeer na Bonde la Sichuan,
wastani wa mwinuko wake kutoka
usawa wa bahari ni mita 1000-2000.
Ukipita ukingo wa mashariki
wa ngazi ya pili ni ngazi
ya tatu inayoundwa na Milima
Daxinganling, Milima Taihan,
Mlima Wu na Mlima Xuefeng
inayoelekea pwani ya mashariki
ya bahari ya Pasifiki. Katika
sehemu ya mwinuko unaotelemka
chini ya mita 500 hadi 1000,
kuna Tambarare ya Kaskazini
ya mashariki, Tambarare ya
Kaskazini, na Tambarare ya
eneo la katikati na chini
ya mtitiriko wa Mto Changjiang,
na katika sehemu ya ukingoni
mwa tambarare hizo kuna milima
mifupi na vilima. Mashariki
ya sehemu hiyo ni sehemu inayoelekea
kwenye bahari ya China yaani
ngazi ya nne, ambapo kimo
cha maji ya sehemu kubwa ni
chini ya mita 200.
|