Mgawanyo wa mikoa ya utawala
中国国际广播电台


       Utaratibu wa sehemu za utawala
Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China inasema kuwa, sehemu za utawala za China zinagawika kama zifuatazo:
( 1 ) Nchi nzima imegawanywa katika mikoa, mikoa inayojiendesha na miji inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu.
( 2 ) Mikoa na mikoa inayojiendesha inagawanyika kuwa majimbo, wilaya, wilaya zinazojiendesha na miji.
( 3 ) Wilaya, wilaya zinazojiendesha na miji inagawanyika kuwa tarafa, tarafa za kikabila na miji ya wilaya.
Mikoa inayojiendesha, majimbo yanayojiendesha na wilaya zinazojiendesha zote ni sehemu zinazojiendesha za makabila madogomadogo.
Serikali kuu inaweza kuanzisha mkoa wa utawala maalum wakati kuna haja ya lazima.
Hivi sasa China ina sehemu 34 za utawala wa ngazi ya mikoa, pamoja na miji minne inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu, mikoa 23, majimbo matano yanayojiendesha, na mikoa miwili ya utawala maalum.