中国国际广播电台
Beijing
Beijing ni mji mkuu wa Jamhuri
ya Watu wa China, ambao unaitwa
pia kuwa Jing kwa ufupi. Beijing
iko kwenye ncha ya kaskazini
magharibi ya Tambarare ya
Huabei. Mwanzoni Beijing iliitwa
kuwa Ji, na ilikuwa mji mkuu
wa Dola la Yan wakati wa madola
ya vita ya Chunqiu, na iliwahi
kuwa mji mkuu wa pili wa Enzi
ya Liao na kuitwa kuwa Yanjing.
Beijing ilikuwa mji mkuu katika
Enzi za Jin, Yuan, Ming na
Qing na mwanzoni mwa Mingguo.
Iliwahi kuitwa kuwa Zhongdu,
Dadu, Beiping na Beijing.
Beijing iliwekwa kuwa mji
kuanzia mwaka 1928. Hivi sasa
mji huo una manispaa 16 na
wilaya mbili, na ni mji unaotawaliwa
moja kwa moja na serikali
kuu. Eneo la mji mzima ni
kilomita za mraba 1.68. Mwishoni
mwa mwaka 2002, idadi ya watu
wenye kadi za ukazi ilikuwa
milioni 11.363. Beijing ni
kituo cha kisiasa cha China
pia ni kituo cha utamaduni,
sayansi na elimu na sehemu
muhimu ya mawasiliano. Aidha,
Beijing ni sehemu yenye vivutio
vingi vya utalii vinavyojulikana
nchini na ng’ambo, vivutio
hivyo ni pamoja na Ukuta mkuu,
masri ya wafalme wa kale,
Bustani ya Tiantan, Makaburi
ya wafalme 13, hekalu la majira
ya joto na Mlima Xiangshan.
Shanghai
Shanghai inaitwa Hu kwa ufupi.
Shanghai iko kwenye sehemu
ya katikati ya pwani ya mashariki
ya China na sehemu ya mlango
wa kuingia baharini kwa maji
ya Mto Changjiang. Katika
zama za kale, sehemu hiyo
ilikuwa kijiji cha wavuvi
cha kando ya bahari, ambayo
ilikuwa sehemu ya Dola ya
Wu wakati wa Enzi ya madola
ya vita ya Chunqiu, na ilikuwa
mji wa wilaya wakati wa Enzi
ya Son, ilianza kuitwa Shanghai,
na kuibuka kuwa mji kuanzia
mwaka 1927. Hivi sasa Shanghai
ni mmoja kati ya miji mikubwa
minne inayotawaliwa moja kwa
moja na serikali kuu ya China,
mji huo una minispaa 18 na
wilaya moja. Eneo la mji mzima
ni kilomita za mraba 5800.
Hadi mwishoni mwa mwaka 2002,
idadi ya watu wa mji huo ilikuwa
milioni 13.347. Shanghai ni
mji mkubwa wa kwanza wa China,
pia ni mmoja kati ya miji
mikubwa duniani. Shanghai
pia ni mji wa viwanda ulio
mkubwa zaidi kuliko mingine
ya China, pia ni kituo cha
biashara, fedha na sayansi
na teknolojia.
Tianjin
Tianjin inaitwa Jin kwa ufupi.
Tianjin iko kwenye sehemu
ya kaskazini mashariki ya
Tambarare ya Huabei, na kwenye
sehemu ya makutano ya matawi
matano ya Mto Huai. Iliitwa
Zhigu katika Enzi ya Jin,
ambayo ilikuwa sehemu muhimu
ya usafiri wa meli, baadaye
iliwekwa kuwa mji wa wilaya
ya Haijin, na mwanzoni mwa
Enzi ya Ming iliitwa kuwa
Tianjin, na ilikuwa mji wa
Tianjin kuanzia mwaka 1928.
Hivi sasa Tinjian ina minispa
15 na wilaya 3, Tinjian ni
mji unaotawaliwa moja kwa
moja na serikali kuu. Eneo
la mji mzima ni kilomita za
mraba zaidi ya elfu 11. Hadi
kufikia mwishoni mwa mwaka
2002, idadi ya watu wa mji
huo ilikuwa milioni 9.1905.
Tianjin ni mji mkubwa kabisa
wa viwanda kwenye sehemu ya
kaskazini ya China, mji huo
una maliasili nyingi ya mafuta
na gesi, na chumvi zilizotengenezwa
kwa maji ya baharini, mji
huo pia una msingi imara kiasi
wa teknolojia za viwanda,
vilevile ni kituo muhimu cha
biashara na bandari katika
sehemu ya kaskazini ya China.
Mji huo una vivutio vya utalii
kama vile Bustani ya Ning,
Jumba la malkia, Kituo cha
mizinga cha Dagu, Hekalu la
Dule la wilaya ya Ji, Ukuta
mkuu wa kale wa mlango wa
Huangya na sehemu ya Mlima
Pang yenye mandhari nzuri.
Chongqing
Chongqing unaitwa Yu kwa ufupi.
Uko mashariki ya sehemu ya
kusini magharibi ya China,
na kwenye eneo la juu la Mto
Changjiang, ilikuwa sehemu
ya Dola la Ba wakati wa Madola
ya vita ya Chunqiu. Chongqing
ilikuwa mji mkuu wa pili wa
serikali ya Chama cha Guomindang
wakati wa kupambana na uvamizi
wa Japan. Mwaka 1997 Chongqing
iliamuliwa kuwa mji unaotawaliwa
moja kwa moja na serikali
kuu, mji huo una minispa 15,
miji midogo minne ya ngazi
ya wilaya, pamoja na wilaya
17 na wilaya 4 inayojiendesha
ya makabila madogomadogo.
Eneo la mji mzima ni kilomita
za mraba elfu 82.3. Hadi kufikia
mwishoni mwa mwaka 2002, idadi
ya jumla ya watu wa mji huo
ilikuwa milioni 31.07. Chongqing
ni mji wa viwada vya mseto,
sehemu hiyo ina vivutio vya
utalii kama vile Magenge matatu
ya Mto Changjian, Mlima Pipa
na Mlima Jinyun.
Hebei
Mkoa wa Hebei unaitwa Ji kwa
ufupi, uko kwenye sehemu ya
kaskazini ya China, mkoa huo
unakaribia na Bahari Bo. Eneo
la mkoa huo ni kilomita za
mraba laki 1.9. Idadi ya watu
ni milioni 67.346. Mji mkuu
wa mkoa huo ni Shijiazhuan.
Shanxi
Mkoa wa Shanxi unaitwa Jin
kwa ufupi, uko kwenye sehemu
ya kaskazini ya China na magharibi
ya Milima Taihang. Eneo lake
ni kilomita za mraba zaidi
ya laki 1.5. Idadi ya watu
ni milioni 32.9371. Mji mkuu
wa mkoa huo ni Taiyuan.
Mongolia ya ndani
Mkoa unaojiendesha wa Mongolia
ya ndani unaitwa Mongolia
ya ndani kwa ufupi, uko kwenye
sehemu ya mipaka ya kaskazini
ya China, upande wake wa kaskazini
unapakana na nchi za Mongolia
na Russia. Eneo lake ni kilomita
za mraba zaidi ya milioni
1.1. Idadi ya watu wake ni
milioni 23.7859. Mji mkuu
wa mkoa huo ni Hulhait.
Liaoning
Mkoa wa Liaoning unaitwa Liao
kwa ufupi, uko kusini mwa
sehemu ya kaskazini ya mashariki
ya China, upande wake wa kusini
unakaribia Bahari Bo na Bahari
Huang, upande wake wa mashariki
unapakana na Korea ya kaskazini.
Eneo lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 1.5. Idadi ya
watu wake ni milioni 42.03.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Shenyang.
Jilin
Mkoa wa Jilin unaitwa kuwa
Ji kwa ufupi, uko katikati
ya sehemu ya kaskazini mashariki
ya China, upande wake wa kusini
mashariki unapakana na Russia
na Korea ya kaskazini. Eneo
lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 1.8. Idadi ya
watu wa mkoa huo ni milioni
26.994. Mji mkuu wa mkoa huo
ni Changchun.
Heilongjiang
Mkoa wa Heilongjiang unaitwa
Hei kwa ufupi, uko kaskazini
kabisa ya sehemu ya kaskazini
mashariki ya China, upande
wake wa mashariki na wa kaskazini
zinapakana na Russia. Eneo
lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 4.6. Idara ya
watu wake ni milioni 38.13.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Harbin.
Jiangsu
Mkoa wa Jiangsu unaitwa Su
kwa ufupi, uko kwenye eneo
la chini la Moto Changjiang
na Mto Hui, na kando ya Bahari
Huang. Eneo lake ni kilomita
za mraba zaidi ya laki moja.
Idadi ya watu wa mkoa huo
ni milioni 71.273. Mji mkuu
wa mkoa huo ni Nanjing.
Zhejiang
Mkoa wa Zhejiang unaitwa Zhe
kwa ufupi, uko katikati ya
sehemu ya mashariki ya China
na kando ya Bahari ya Dong.
Eneo lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki moja. Idadi
ya watu wake ni milioni 46.47.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Hangzhou.
Anhui
Mkoa wa Anhui unaitwa Wan
kwa ufupi, ambao uko kaskazini
magharibi ya sehemu ya mashariki
ya China, mkoa huo unapita
Mto Changjiang na Mto Huai.
Eneo lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 1.3. Idadi ya
watu wake ni milioni 63.68.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Hefei.
Fujian
Mkoa wa Fujian unaitwa Min
kwa ufupi, uko kwenye pwani
ya kusini mashariki ya China,
mkoa huo unakabiliana na mkoa
wa Taiwan kwa bahari. Eneo
lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 1.2. Idadi ya
watu wake ni milioni 34.66.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Fuzhou.
Jiangxi
Mkoa wa Jiangxi unaitwa Gan
kwa ufupi, uko kwenye kando
ya kusini ya eneo la katikati
na la chini la Mto Changjiang.
Eneo la mkoa huo ni kilomita
za mraba zaidi ya laki 1.6.
Idadi ya watu wake ni milioni
42.2243. Mji mkuu wa mkoa
huo ni Nanchang.
Shandong
Mkoa wa Shandong unaitwa Lu,o
uko kwenye eneo la chini la
Mto Huang, unakaribia Bahari
Huang na Bahari Bo. Eneo lake
ni kilomita za mraba zaidi
ya laki 1.5. Idadi ya watu
wake ni milioni 90.82. Mji
mkuu wa mkoa huo ni Jinan.
Henan
Mkoa wa Henan kwa ufupi unaitwa
Yu, uko kwenye eneo la katikati
na la chini ya Mto Huang,
ulikuwa sehemu ya “Zhongyuan”
katika zama za kale. Eneo
lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 1.6. Idadi ya
watu wake ni milioni 96.13.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Zhengzhou.
Hubei
Mkoa wa Hubei unaitwa E, ambao
uko katika eneo la katikati
la Mto Changjiang, na kaskazini
ya Ziwa Dongting. Eneo lake
ni kilomita za mraba zaidi
ya laki 1.8. Idadi ya watu
wake ni milioni 59.878. Mji
mkuu wa mkoa huo ni Wuhan.
Hunan
Mkoa wa Hunan unaitwa Xiang,
ambao uko kwenye kando ya
kusini ya eneo la katikati
ya Mto Changjiang, sehemu
kubwa ya mkoa huo iko kusini
ya Ziwa Dongting. Eneo la
mkoa huo ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 2.1. Idadi ya
watu wake ni milioni 66.285.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Changsha.
Guangdong
Mkoa wa Guangdong unaitwa
Yue, ambao uko kusini mwa
Mlima Nanling, na kwenye kando
ya Bahari ya kusini. Eneo
lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 1.8. Idadi ya
watu wake ni milioni 78.5858.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Guangzhou.
Guangxi
Mkoa unaojiendesha wa kabila
la wazhuan wa Guangxi unaitwa
Gui kwa ufupi, uko magharibi
ya sehemu ya kusini ya China,
upande wake wa kusini unakaribia
Ghuba ya Beibu, sehemu ya
kusini magharibi ya mkoa huo
inapakana na Vietnam. Eneo
la mkoa huo ni kilomita za
mraba zaidi ya laki 2.3. Idadi
ya watu wake ni milioni 48.22.
Mji mkuu ni Nanning.
Hainan
Mkoa wa Hainan unaitwa Qiong,
ambao uko pwani ya kusini
mwa China, upande wake wa
kaskazini unakabiliana na
Mkoa wa Guangdong, kati yao
ni Mlango wa bahari wa Qiongzhou.
Mkoa huo una Kisiwa cha Hainan,
Visiwa vya Xisha, Visiwa vya
Nansha, Visiwa vya Zhongsha
na eneo lake la mamlaka ya
bahari. Eneo la nchi kavu
la mkoa huo ni kilomita za
mraba zaidi ya elfu 34. Idadi
ya watu wake ni milioni 8.0313.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Haikou.
Sichuan
Mkoa wa Sichuan unaitwa Chuan
au Shu, ambao uko kwenye sehemu
ya kusini magharibi ya China
na eneo la juu la Mto Changjiang.
Eneo lake ni kilomita za mraba
laki 4.8. Idadi ya watu wake
ni milioni 86.733. Mji wake
mkuu ni Chengdu.
Guizhou
Mkoa wa Guizhou kwa ufupi
unaitwa Qian au Gui, uko mashariki
ya Uwanda wa juu wa Yunnan
na Guizhou wa kusini magharibi
ya China. Eneo lake ni kilomita
za mraba zaidi ya laki 1.7.
Idadi ya watu wake ni milioni
38.3728. Mji mkuu wa mkoa
huo ni Guiyang.
Tibet
Mkoa unaojiendesha wa Tibet
unaoitwa Zang, uko kwenye
Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet,
na unapakana na India, Nipel,
Buthan, na Myanmar. Eneo lake
ni zaidi ya kilomita za mraba
120, idadi ya watu wake ni
milioni 2.63. Mji mkuu wake
ni Lahsa.
Yunnan
Mkoa wa Yunnan unaitwa Dian
au Yun, uko kwenye sehemu
ya mpaka wa kusini magharibi
ya China, na unapakana na
Myanmar, Laos na Vienam. Eneo
lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 3.8. Idadi ya
watu wake ni milioni 43.331.
Mji mkuu wake ni Kunming.
Shanxi
Mkoa wa Shanxi unaitwa Shan
au Qin,uko kwenye eneo la
katikati ya Mto Huanghe. Eneo
lake ni kilomita za mraba
zaidi ya laki 1.9. Idadi ya
watu wake ni milioni 36.737.
Mji mkuu ni Xian.
Gansu
Mkoa wa Gansu unaitwa Gan
au Long, ambao uko kwenye
eneo la katikati la Mto Huang,
kaskaizni magharibi ya China,
sehemu moja ya upande wake
wa kaskazini magharibi inapakana
na Mongolia. Eneo lake ni
kilomita za mraba zaidi ya
laki 3.9. Idadi ya watu wake
ni milioni 25.9258. Mji mkuu
ni Lanzhou.
Qinghai
Mkoa wa Qinghai unaitwa Qing,
ambao uko kaskazini magharibi
ya China na kwenye eneo la
juu la Mto Changjiang na Mto
Huanghe. Eneo lake ni kilomita
za mraba zaidi ya laki 7.2.
Idadi ya watu wake ni milioni
5.286. Mji mkuu wa mkoa huo
ni Xining.
Ningxia
Mkoa unaojiendesha wa kabila
la wahui wa Ningxia unaitwa
Ning, ambao uko kwenye eneo
la katikati la Mto Huanghe,
kaskazini magharibi ya China.
Eneo lake ni kilomita za mraba
zaidi la elfu 66. Idadi ya
watu wake ni milioni 5.7154.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Yinchuan.
Xinjiang
Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang
Uyrgu unaitwa Xin, ambao uko
kwenye sehemu ya mipaka ya
kaskazini magharibi ya China,
mkoa huo unapakana na Mongolia,
Russia, Kazakstan, Kyrgyzstan,
Tajikstan, Afghanistan, Pakistan
na India. Eneo lake ni kilomita
za mraba zaidi ya milioni
1.6, ni mkoa wenye eneo kubwa
zaidi kuliko mingine nchini
China. Idadi ya watu wake
ni milioni 19.0519. Mji mkuu
wa mkoa huo ni Urmuqi.
Taiwan
Mkoa wa Taiwan unaitwa Tai,
ambao uko kwenye sehemu ya
rafu inayoelekea pwani ya
kusini mashariki ya China,
Taiwan ni kisiwa kikubwa cha
kwanza cha China, upande wake
wa mashariki unakaribia Bahari
ya Pasifiki, kaskazini mashariki
inapakana na Visiwa vya Liuqiu,
kusini kupakana na Mlango
wa bahari wa Bash. Sehemu
yake ya kusini inakabiliana
na Mkoa wa Fujian, kati yao
ni Mlango wa bahari wa Taiwan.
Eneo lake ni kilomita za mraba
elfu 36. Idara husika ya Taiwan
ilitoa takwimu zikionesha
kuwa, hadi mwezi Agosti mwaka
2002, idadi ya watu wa Mkoa
wa Taiwan ni zaidi ya milioni
22.4, na idadi ya jumla ya
watu wake ni milioni 22.48
wakiwemo watu wa Jinmen na
Mazu. Mji mkuu wa Mkoa wa
Taiwan ni Taibei.
Hongkong
China ilirudisha mamlaka yake
huko Hongkong kuanzia tarehe
1 Julai mwaka 1997, na ikaanzisha
Mkoa wa utawala maalum wa
Hongkong. Hongkong inaitwa
Gang kwa ufupi , ambao uko
kwenye pwani ya Bahari ya
kusini na upande wa mashariki
ya Mlango wa Mto Zhujing,
kusini ya mji Shenzhen wa
Mkoa wa Guangdong. Hongkong
ina kisiwa cha Hongkong, visiwa
vya Jiulong na Xinjie pamoja
na vingine vilivyoko karibu
navyo. Eneo la jumla la Hongkong
ni kilomita za mraba 1098.51.
Ilipofika mwishoni mwa mwaka
2002, idadi ya jumla ya watu
wa Hongkong ilikuwa milioni
6.8158, miongoni mwao wakazi
wa kudumu ni milioni 6.6253,
na wakazi wanaohamahama ni
laki 1.905 .
|