中国国际广播电台
China ina utajiri mkubwa wa
madini, na utajiri huo umethibitishwa
kuwa ni 12% ya utajiri wote
wa madini duniani, na China
ni nchi ya tatu yenye utajiri
mkubwa wa madini duniani.
Hata hivyo, wastani wa umiliki
wa madini wa kila Mchina ni
58% tu ya ule wa duniani,
wastani huo wa umiliki wa
madini kwa kila Mchina unachukua
nafasi ya 53 duniani. Hadi
sasa madini aina 171 yamegunduliwa
na aina 158 zimethibitishwa
utajiri wao (aina za nishati
10, aina za metali nyeusi
5, metali za rangi 41, madini
yenye metali thamani 8 na
madini yasiyo ya metali 91
na madini ya maji na gesi
aina 3). China ni moja ya
nchi chache zenye utajiri
mkubwa wa madini, aina nyingi
za kikamilifu za madini. Kutokana
na utajiri uliothibitishwa,
aina 25 kati ya aina 45 muhimu
zilizopatikana nchini China
zinachukua nafasi ya tatu
duniani, na kati ya aina hizo
25 madini ya udongo adimu,
jasi, vanadium, titanium,
tantalum, wolfram, kinywe,
shura, barite, magnesite,
antimony yanachukua nafasi
ya kwanza duniani.
Utapakaaji wa madini nchini
China ni kama ifuatavyo: Mafuta
na gesi asilia yanapatikana
kwa wingi zaidi katika sehemu
ya kaskazini-mashariki, kaskazini
na kaskazini-magharibi ya
China. Makaa ya mawe yanapatikana
zaidi katika sehemu ya kaskazini,
na kaskazini-magharibi ya
China. Madini ya chuma yako
zaidi katika sehemu ya kaskazini-mashariki,
kaskazini na kusini-magharibi
ya China. Madini ya shaba
mengi zaidi yako katika sehemu
ya kusini-magharibi, kaskazini-magharibi,
na mashariki ya China. Madini
ya risasi na zinki yanapatikana
kote nchini China, na madini
ya wolfram, risasi, molybdenum,
antimony, na udongo adimu
yanapatikana zaidi katika
sehemu ya kusini, kaskazini
mwa China. Madini ya dhahabu
na fedha yanapatikana kote
nchini na kisiwani Taiwan.
Madini ya phosphorus yanapatikana
zaidi katika sehemu ya kusini
ya China.
Maliasili ya madini muhimu
nchini China ni yafuatayo:
Makaa ya mawe: China inaongoza
kwa utajiri wa makaa ya mawe
duniani. Makaa ya mawe yamethibitishwa
kuwa ni tani bilioni 1000
ambayo mengi zaidi yako katika
sehemu ya kaskazini, kaskazini-magharibi
na hasa katika mikoa ya Shanxi,
Shan’xi na Mongolia ya Ndani.
Mafuta na gesi: Mafuta na
gesi zaidi ziko katika sehemu
ya kaskazini-magharibi, sehemu
ya kaskazini-mashariki, kaskazini
na sehemu ya mwambao wa mashariki
ndani ya bahari. Hadi kufikia
mwishoni mwa mwaka 1998 maeneo
509 ya mafuta na maeneo 163
ya gesi yaligunduliwa nchini
China. Utajiri wa mafuta umethibitishwa
kuwa ni tani bilioni 18.85
ikiwa ni nafasi ya tisa duniani
na gesi mita za ujazo bilioni
1950 ikiwa ni nafasi ya 20
duniani. Na mafuta na gesi
yaliyoko China bara ni 73.8%
na 78.4% ya utajiri wote wa
maliasili hiyo.
Madini ya metali:
Metali nyeusi: China imethibitishwa
kuwa na utajiri wa chuma,
manganese, vanadium na titanium,
na kati ya metali hizo, kiasi
cha chuma ni tani bilioni
50, kiasi kikubwa kinapatikana
katika mikoa ya Liaoning,
Hebei, Shanxi na Sichuan.
Metali zenye rangi:
Metali zenye rangi zilizogunduliwa
duniani zote zinaweza kupatikana
pia nchini China, na kati
ya metali hizo udongo adimu
unachukua 80% ya dunia nzima
na utajiri wa antimony unachukua
40% duniani na utajiri wa
wolfram ni mara nne kuliko
utajiri wa metali hiyo katika
nchi zote nyingine kwa pamoja.
|