中国国际广播电台
Halikadhalika, China pia ni
nchi yenye aina nyingi za
mimea, kiasi cha aina elfu
30 za mimea zinapatikana nchini
China, ni nchi ya tatu kwa
kuwa na aina nyingi za mimea
ikizifuata Malaysia na Brazil.
Mimia ya jamii za bryophyte
ni 70% ya aina zote zipatikanazo
duniani na pteridophyte aina
2600 katika jamii 52 ambazo
ni 80% ya aina zote zipatikanazo
duniani, na aina 8 za miti
ya mbao na aina 2,000 za miti.
Hapa duniani kuna aina 750
za mbegu zisizo na gamba la
nje, aina 240 kati ya hizo
zinaweza kupatikana pia nchini
China. Miti yenye majani kama
ya sindano inachukua 37.8%
katika aina zote za miti hiyo
duniani.
Mimea inayoota katika nusu
ya dunia ya kaskazini karibu
yote inaonekana pia nchini
China, kuna mimea elfu 2 ya
chakula, na mimea elfu 3 ya
dawa.
Aina za misitu zinatofautiana
kutoka kaskazini hadi kusini
kutokana na tofauti za hali
ya hewa, misitu ya aina zote
ya ukanda wa baridi, wenye
jotoridi wastani, ukanda wenye
joto wastani na ukanda wa
tropiki inapatikana.
|