中国国际广播电台
China ni nchi inayoongoza
duniani kwa idadi ya watu,
kufikia mwishoni mwaka 2002,
idadi ya watu wa China ilikuwa
ni bilioni 1.28453 mbali na
idadi ya watu wa mikoa ya
Hong Kong, Macau na Taiwan.
Hii ni wastani wa moja kwa
tano ya watu wote duniani.
China pia ni nchi yenye watu
wengi kwa wastani wa eneo,
kwa wastani kuna watu 135
katika kila eneo la kilomita
moja. Lakini watu hawapatikani
kwa wastani katika kila sehemu
bali wengi wanakusanyika katika
sehemu ya mashariki, wachache
katika sehemu ya magharibi.
Katika sehemu ya mashariki
kwenye mwambao, kwa wastani
kila katika eleo la kilomita
moja kuna watu zaidi ya 400,
katika sehemu ya katikati
kuna watu 200 na katika sehemu
ya magharibi katika kila eneo
la kilomita moja watu hawafiki
10. Hivi sasa wastani wa kuishi
kwa wananchi wa China umeongezeka
na kuwa miaka 71.4 ( miaka
69.63 kwa wanaume na 73.33
kwa wanawake), umri huo unazidi
wastani wa umri wa kuishi
duniani kwa miaka mitano,
na unazidi nchi zanazoendelea
kwa miaka 7, lakini unapungua
kwa miaka mitano ukilinganishwa
na nchi zilizoendelea.
Mwaka 2002 mwendo wa ongezeko
la idadi ya watu wa China
ulizidi kupungua, mwishoni
mwa mwaka huo idadi ya watu
ulikuwa bilioni 1.28453. Miongoni
mwa watu hao, wakazi wa mijini
ni milioni 502.12 ambao ni
39.1% ya watu wote; watu wa
sehemu za vijijini walikuwa
milioni 782.41 ambao ni 60.9
ya watu wote. Idadi ya wanaume
ni milioni 661.15 na wanawake
milioni 623.38. Watoto kutoka
umri wa miaka sifuri hadi
14 ni 22.4%, wenye umri wa
miaka tokea miaka 15 hadi
64 ni 70.3%, wazee wenye zaidi
ya umri wa miaka 65 ni 7.3%,
idadi ya wazee imefikia milioni
milioni 93.77. Watoto waliozaliwa
katika mwaka 2002 walikuwa
milioni 16.47, ambao ni wastani
wa 12.86 kwa 1000 ya watu
wote; waliokufa walikuwa milioni
8.21, ambao ni wastani wa
watu 6.41 katika 1,000; ongezeko
la watu lilikuwa milioni 8.26,
ambao ni sawa na watu 6.45
kwa kila watu 1000.
|