中国国际广播电台
Uzazi wa mpango ni sera ya
kimsingi ya kitaifa nchini
China. Uzazi wa mpango unatekelezwa
kwa njia ya muunganisho wa
uongozi wa kiserikali na hiari
ya umma. Uongozi wa serikali
unamaanisha kuwa serikali
kuu pamoja na serikali za
mitaa zinatoa sera na mpango
wa ujumla katika udhibiti
wa ongezeko la idadi ya watu,
kuinua ubora wa idadi ya watu,
kuboresha miundo ya idadi
ya watu, na kutoa huduma za
afya ya uzazi, kupata uzazi
bora na malezi bora. Hiari
ya umma inamaanisha kuwa wanaofikia
umri wa kupata watoto wapange
mimba na kuzaa kwa kuzingatia
umri, hali ya afya, kazi na
uchumi wa familia chini ya
mwongozo wa sera na sheria
za kitaifa, na kuchagua njia
inayofaa kuepuka uja uzito.
Sera kuhusu uzazi wa mpango
zinazotumika sasa nchini China
ni kuchelewesha umri wa ndoa
na uja uzito, kuzaa kwa watoto
wachache na malezi bora; na
mume na mke kuzaa mtoto mmoja
tu. Katika sehemu za vijijini,
mume na mke wakiwa kweli wana
shida fulani wanaruhusiwa
kuzaa watoto wawili; na katika
sehemu za makabila madogo
madogo sera ni tofauti kutokana
na hali tofauti ya idadi ya
watu, maliasili, uchumi, utamaduni
na mila, kwamba kwa kawaida
mume na mke wanaweza kuzaa
watoto wawili na katika sehemu
nyingine wanaweza kuzaa watoto
watatu, na kabila lenye idadi
ndogo sana ya watu wa kabila
fulani hawawekewi kikomo cha
watoto.
Tokea sera za uzazi wa mpango
zianze kutekelezwa, kuchelewesha
umri wa kuoa, kuzaa, kuzaa
watoto wachache na kutoa kwa
malezi bora imekuwa desturi
katika jamii. Pamoja na hayo
uzazi wa mpango umewawezesha
wanawake kujinasua kuzaa mara
nyingi na adha za nyumba,
hali ya afya ya watoto na
mama wazazi pia imekuwa bora
zaidi.
|