Mazingira ya Kijiografia

中国国际广播电台

      Xinjiang iko katika sehemu ya ndani ya Asia, kutoka upande wa kaskazini hadi upande wake wa kusini kuna milima ya Aertai, Tian na Kunlun pamoja na mabonde ya Zhungeer na Tulufan kati ya milima hiyo. Watu wamezoea kuiita sehemu ya kusini ya mlima wa Tian kuwa “Xinjiang ya Kusini”, na sehemu ya kaskazini ya mlima wa Tian kuwa “Xinjiang ya Kaskazini” na kuita mabonde ya Hami na Tulufan “Xinjiang ya Mashariki”. Miji na vijiji vya Xinjiang vyote viko pembezoni mwa mabonde mawili kama mkufu wa lulu.

Mkoani Xinjiang kuna mto Talimu, ambao ni wa kwanza kwa urefu kwenye sehemu ya ndani ya bara, pamoja na ziwa la Bositeng lenye maji baridi, ambalo ni la kwanza kwa ukubwa kwenye sehemu ya ndani ya bara na bonde la Tulufan, ambalo ni la kwanza kwa kuinama chini kabisa nchini China. Xinjiang iko kwenye sehemu yenye ukame na yenye tofauti kubwa sana kati ya hali joto ya mchana na usiku, sehemu ya Aletai ina rekodi kuwa na hali joto baridi kabisa, wakati sehemu ya Tulufan inakwenda kinyume chake kabisa nchini China.
Theluthi mbili za eneo la jangwa nchini China ziko mkoani Xingjian, ambayo eneo la jangwa la Takelamagan ni kilomita za mraba elfu 33, ni la kwanza kwa ukubwa nchini na ni jangwa la pili kwa ukubwa linalohamahama duniani. Jangwa la Guerbantonggute lililoko kwenye bonde la Zhungeer lina eneo la kilomita za mraba elfu 48, ambalo ni la pili kwa ukubwa hapa nchini. Katika majangwa ya nchini kuna rasilimali nyingi za mafuta ya asili ya petroli na gesi asili.

Milima yenye theluji na barafu mkoani Xingjian imekuwa chimbuko la maji ya mito. Wastani wa rasilimali wa mkazi wa Xingjian unachukua nafasi ya mbele nchini.