中国国际广播电台
Kabla ya miaka zaidi ya 2,000
iliyopita, Xinjiang ilikuwa
moja ya sehemu ya umoja wa
makabila mengi ya China. Mwaka
60 KK, enzi ya Han ilianzisha
serikali kwenye eneo la magharibi,
ambapo Xinjiang ilisimamiwa
moja kwa moja na utawala wa
enzi ya Han ya magharibi,
na eneo lake lilikuwa pamoja
ziwa la Baerkashi na sehemu
ya Pamier ya hivi sasa. Katika
muda wa miaka zaidi ya 1,000
hapa baadaye, sehemu ya Xinjiang
imekuwa ikidumisha uhusiano
wa kuwa himaya ya serikali
kuu ya China, ambayo vitengo
vya utawala vilivyowekwa na
serikali kuu vimekuwa vikisimamia
shughuli za Xinjiang.
Katika enzi ya Qing, miaka
zaidi ya 300 iliyopita, serikali
kuu ilimweka jemedari wa Yili
kwenye mji wa Huiyuan, sehemu
ya Yili, Xinjiang, ambaye
alitawala eneo lote la Xinjiang.
Mwaka 1884, ulianzishwa mkoa
wa Xinjiang, ambapo uhusiano
kati yake na mikoa mingine
ya China uliimarishwa zaidi.
Mwezi Septemba mwaka 1949,
Xinjiang ilipata uhuru kwa
njia ya amani. Tarehe 1 mwezi
Oktoba mwaka huo huo ilianzishwa
Jamhuri ya Watu wa China,
ni kama mikoa mingine ya China
Xinjiang ilikuwa mkoa unaojiendesha
kikabila nchini China.
|