中国国际广播电台
Xinjiang ina rasilimali tele,
kiasi cha makaa ya mawe na gesi
ya asili ni theluthi moja ya
idadi ya jumla vitu hivyo vilivyogunduliwa,
gesi ya asili pia ni nyingi
na kuchukua nafasi ya kwanza
katika sehemu ya kaskazini magharibi
ya China. Inakadiriwa kuwa kwenye
eneo lenye mafuta na gesi la
kilomita za mraba elfu 740,
kuna mafuta ya asili ya petroli
tani bilioni 20.8 na mita za
ujazo trilioni 1 ya gesi ya
asili zikiwa ni kiasi cha 30%
ya jumla ya rasilimali za mafuta
na gesi ya asili zilizoko kwenye
nchi kavu na kusifiwa na wataalam
wa China na wa nchi za nje kuwa
ni “bahari yenye matumaini”
ya sekta ya usafishaji wa mafuta
ya petroli nchini. Mradi wa
kupeleka gesi ya asili ya sehemu
ya magharibi kwa sehemu ya mashariki
ya China, ambao ujenzi wake
utakamilika mwezi Oktoba mwaka
huu, na utasafirisha kiasi kikubwa
cha gesi kwenye sehemu ya mashariki
ya China ikiwemo mji wa Shanghai
na sehemu ya pembezoni mwake.
Rasilimali ya makaa ya mawe
ya Xinjiang ni kiasi cha tani
elfu 20, kiasi hicho ni kama
40% ya jumla ya raslimali
ya makaa ya mawe nchini ikichukua
nafasi ya kwanza kwa wingi
wa makaa ya mawe hapa nchini.
|