Kazi za Viwanda za Xingjiang

中国国际广播电台

      Hivi sasa uchumi wa viwanda mkoani Xinjiang umekuwa na ongezeko la kasi, Xinjiang imekuwa na mfumo kamili wa kazi za viwanda zikiwa ni pamoja na chuma, chuma cha pua, makaa ya mawe, mafuta ya asili ya petroli, mitambo, kemikali, vifaa vya ujenzi, nguo, sukari, karatasi, ngozi na sigara. Kwa kutumia hali bora ya rasilimali za mkoa huo, Xinjiang imeanzisha sekta za uzalishaji mali wenye umaalumu wa Xinjiang. Hivi sasa, Xinjiang imekuwa na viwanda zaidi ya elfu 60 vya aina mbalimbali vya kazi za usafishaji wa mafuta ya asili ya petroli, makaa ya mawe, uyeyushaji wa madini, umeme, nguo, kemikali, mitambo, vifaa vya ujenzi na chakula, ambavyo vinazalisha bidhaa za aina zaidi ya 2,000.