Kilimo cha Xinjiang

中国国际广播电台

      Xinjiang ina mwangaza mwingi wa jua pamoja na ardhi kubwa. Wakazi wa huko wameendeleza kilimo kwenye sehemu zenye maji. Mazao ya kilimo ya Xinjiang ni pamoja na ngano, mahindi na mpunga. Mazao ya kiuchumi ni pamoja na pamba, mboga za kutengenezea sukari na maua ya kutengenezea bia. Kati ya mazao hayo ya kilimo, uzalishaji wa pamba unachukua nafasi muhimu nchini China, tena pamba hiyo ina nyuzi ndefu, ambazo ubora wake unalingana na pamba maarufu za Misri.
Xinjiang pia inajulikana kwa uzalishaji wa matunda na matikiti ya aina mbalimbali yakiwemo zabibu, matikiti ya Hami, matikiti ya maji, matufaha, mapea, mapichi, mapera, maaprokoti na matunda mengine, lakini zabibu na matikiti ya Hami ni matamu sana. Katika miaka ya karibuni kilimo cha Xinjiang kimeendelezwa kuwa kwa haraka na kuwa sekta kubwa yenye kazi za uzalishaji na usindikaji.