Xinjiang
ina mifugo ya aina nyingi na
ni moja ya sehemu muhimu ya
ufugaji. Toka zamani, Xingjian
ni sehemu inayozalisha farasi
bora na wanyama wengine kama
ng’ombe, kondoo, punda ngamia
na yak. Uzalishaji wa nyama
ya kondoo wa Xinjiang unachukua
nafasi ya pili nchini China,
idadi ya mifugo ni zaidi ya
milioni 40.
Eneo la mbuga ya malisho yenye
majani mkoani Xinjiang ni kilomita
kiasi cha elfu 570 ikichukua
87% ya maeneo ya kilimo, misitu
na malisho ya mifugo. Rasilimali
ya malisho yenye majani ni muhimu
ya na ya kimsingi kwa uendelezaji
wa ufugaji wa mifugo mkoani
Xinjiang, ambayo kiasi cha 70%
ya mifugo ya Xinjiang inategemea
majani yake. Xinjiang ni kituo
cha uzalishaji wa aina bora
na mpya za mifugo nchini China.