Kabila la Wauigur

中国国际广播电台

     Kabila la wauigur ni moja ya makabila yaliyokuweko toka zamani za kale, “uigur” ni jina wanalojiita, ambalo maana yake ni “umoja” au muungano”. Kabila la wauigur, ambalo idadi ya watu inazidi milioni 7, ni kubwa kwenye sehemu ya Xinjiang,. Kabila hilo la watu lina lugha na maandishi yake.
Mavazi ya jadi ya wauigur ni kuwa wanaume kwa wanawake na wazee kwa watoto wote wanapenda kuvaa makofia ya pembe nne na yenye nakshi za kutariziwa. Wanaume wanapenda kuvaa kanzu na shati ndani yake. Wanawake wanapenda kuvaa gauni na vizibau vyeusi nje, kuvaa hereni, bangili, pete na mikufu, wasichana wanapenda sana kusuka nywele zenye mikia mingi. Wakazi wa mijini hivi sasa wanavaa mavazi ya kisasa.
Watu wa kabila la wauigur wana adabu kubwa, wanapoona wazee au marafiki, wanazoea kuweka mikono yao ya kulia kwenye katikati ya kifua na kuinama kwa mbele huku wanawasalimia.