Idadi ya watu wa kabila la watadzhik
mkoani Xinjiang imefikia zaidi
ya elfu 36, na wengi wao wanaishi
kwenye wila inayojiendesha ya
Tadzhik. Watu wengi wa kabila
hilo ni wafugaji na pia wanafanya
shughuli za kilimo. Tangu karne
nyingi zilizopita walikuwa wamejenga
makazi yao kwenye mabonde yenye
urefu wa mita kiasi cha 3,000
juu ya usawa wa bahari, wanapanda
mbegu za mazao yanayovumilia
baridi katika majira ya Spring,
kisha wanaswaga mifugo yao kwenye
malisho yenye majani yaliyoko
kwenye milima, ikifika majira
ya kupukutika majani wanarejea
vijijini kuvuna mazao waliyopanda
na kukaa nyumbani katika siku
za baridi kali, wanaishi hivyo
mwaka nenda na mwaka rudi. Mwanaume
anapenda kuvaa kanzu ndefu isiyo
na ukosi na kufunga mkanda kiunoni,
katika siku za baridi anavaa
koti refu na kofia ndefu iliyoshonwa
kwa ngozi ya kondoo. Wanapenda
kula samli na vyakula vilivyotengenezwa
kwa maziwa.
Watu wa kabila la watadzhik
wanayo lugha na maandishi yao.
Wanapocheza ngoma huiga mwewe
anavyoruka. Mwewe ni alama ya
ushujaa, hivyo watu wa kabila
hilo wanaita kabila lao ni la
mwewe.