中国国际广播电台
Mji wa kale wa Loulan uko
katika sehemu ya kaskazini
magharibi ya Luobubo, kusini
mwa Xinjiang, ambao ulikuwa
mji muhimu sana kwenye njia
ijulikanayo kwa “njia ya hariri”
hapo zamani. Hivi sasa mji
huo umezungukwa na jangwa
na chumvi iliyoganda imara,
sehemu hiyo imekuwa pori lenye
hatari na kutoonekana watu.
Kutokana na vitabu vya historia,
mnamo karne ya 2 kabla ya
Kristo, Loulan ilikuwa moja
ya sehemu iliyoendelea sana
kwenye sehemu ya magharibi
ya China. Kitu kinachoshangaza
ni kwamba dola hilo, ambalo
jina lake lilivuma sana, lilitoweka
ghafla baada ya kustawi kwa
miaka zaidi ya mia 5 au 6.
Mji wa kale wa Loulan ulitoweka
namna gani? Toka muda mrefu
uliopita, suala hilo jambo
hilo lilikuwa suala linalofuatiliwa
na watafiti wa mambo ya kale
na wanasayansi. Loulan pamekuwa
mahali penye siri na ajabu
panapovutia watu wanaotaka
kuvumbua siri ya maumbile
ya asili duniani.
Kutokana na uchunguzi uliofanywa
kuhusu mji wa kale wa Loulan,
mji huo ulitoweka kwa kufunikwa
na jangwa kutokana na chanzo
cha kimaumbile na shughuli
za binadamu ambazo zilifanya
maji ya mto kutiririka kwa
kubadilisha njia yake. Kutokana
na uchunguzi kuwa mji wa kale
wa Loulan ulikuwa na eneo
la mita za mraba elfu 120,
ambao kuta za mji huo zilitengenezwa
kwa udongo, matete (bulrush)
na vijiti vya miti. Mto mmoja
karibu ulipitia katikati ya
mji huo kutoka upande wa kaskazini
magharibi hadi upande wa kusini
mashariki, lakini vilivyobaki
hadi hivi sasa ni mnara wa
dini ya kibudha pamoja na
majengo yaliyoko karibu na
mnara huo. Karibu na mji huo
kuna mabaki ya mnara wa kupasha
habari wakati wa dharura,
maghala ya nafaka na makaburi.
Ndani ya makaburi ya mji wa
Loulan ilifukuliwa maiti kavu
ya “mrenbo wa Loulan” ya kabla
ya miaka 3,800 iliyopita.
Sasa ndani ya mji wa kale
wa Loulan bado kuna mabaki
ya vipande vya vyungu vya
zamani, maturubai ya sufu,
nguo zilizochanika na kuoza
za hariri pamoja na pesa za
shaba na silaha za kale
|