Kwenye “njia ya hariri” ndefu
ya kuelekea Xinjiang kuna mabaki
ya majengo ya ngome yanayojulikana
duniani, malango ya njia, hekalu
la pango la mawe, nyumba za
wageni, makaburi na minara ya
kupasha habari wakati usalama
unapotishiwa.
Pango lenye sanamu za kibudhaa
elfu moja lililoko Kezier na
pango la sanamu za kibudha elfu
moja lililoko Baizikelike ni
mapango maarufu zaidi kutokana
na sanamu na mapicha yaliyochongwa
na kuchorwa kwenye kuta za pango
la mawe ambazo zimeunganisha
utamaduni wa China, India na
uajemi na kuonesha hali ya uzalishaji
mali na maisha ya wakati wa
makabila mbalimbali.
Mapango hayo yalitobolwa toka
karne ya 6 hadi karne ya 14
kaskazini mashariki ya mji wa
Turufan ingawa baadhi ya sanamu
na mapicha kwenye kuta za mapango
yameharibiwa, lakini eneo linalohifadhiwa
bado limefikia mita za mraba
zaidi ya 1,200, ambapo panatambuliwa
kuwa ni mahali panapohifadhiwa
vizuri zaidi penye sanaa za
dini ya kibudha duniani.