Tulufan
中国国际广播电台  

Kwenye bonde linaloinama chini sana, sehemu ya kati ya Xinjiang kuna mahali panapojulikana kama “ardhi ya moto”, sehemu hiyo inaitwa kwa jina na Tulufan. Kutokana na hali maalumu ya kijiografia, Tulufan ina maji mengi chini ya ardhi, hivyo ni mahali pazuri kwa ukuaji wa mizabibu, matikiti maji na matunda mengine. Kutokana na uhaba wa mvua, matunda yanayozalishwa huko ni matamu zaidi, kuna watalii wengi wanaokwenda huko kwa lengo la kula matunda.