Jina kamili la Kashi ni “Kashigeer”,
sehemu hiyo inasifiwa kuwa ni
“lulu iliyoko kwenye njia ya
hariri” na ni mji wa kale wenye
utamaduni wa miaka mingi.
Kashi ni sehemu yenye maji na
mimea kwenye upande wa magharibi
wa bonde la Talimu tangu zamani
za kale.
Sehemu ya Kashi ina raslimali
kubwa ya utalii kutokana na
mandhari yake nzuri, jangwa,
milima yenye barafu na theluji
pamoja na milima mizuri.
Kashi inavutia sana watalii
kutokana na utamaduni na majengo
maalumu wa kiurgur, hata watu
wamesema kuwa “mtu asiyefika
Kashi haonekani kama amefika
Xinjiang”.