Xinjiang ni mahali pekee duniani
penye aina nne kubwa za dini
ya kibudha, kijing, kimoni na
kiislam. Mnamo karne ya kwanza,
dini ya kibudha ilienezwa hadi
sehemu ya mashariki kwa kufuata
njia ya hariri na kufikia sehemu
nyingi za China. Dini ya kijing
ni dhahebu moja la dini ya kikristu,
ambalo liliingia Xinjiang katika
karne ya 6. Utafiti uliofanywa
kuhusu mambo ya kale unaonesha
kuwa dini ya kijing ilienea
sana huko Xinjiang, na kuwa
moja ya kituo cha dini hiyo,
isipokuwa ilianza kufifia baada
ya dini ya kiislam kuingia huko
hapo baadaye. Katikati ya karne
ya 10, dini ya kiislam iliingia
Kashi kwa kufuata njia ya hariri,
na ilienea sana kwenye sehemu
ya Xinjiang kati ya karne ya
16 hadi karne ya 17. Hivi sasa
wengi wa watu wa makabila kumi
ya Xinjiang ni waumini wa dini
ya kiislam.