Mkoa
wa Tibet ni moja ya mikoa mitano
inayojiendesha yenyewe nchini
China, kwa ufupi mkoa huo unaitwa
kuwa Tibet. Tibet iko katika
sehemu ya kusini magharibi ya
China ikipakana na nchi za Myanmar,
India na Bhutan na Nepal kwenye
upande wake wa kusini na upande
wa magharibi, urefu wa mpaka
unakaribia kilomita 4,000. Eneo
la Tibet ni kiasi cha kilomita
za mraba milioni 1.22 likichukua
12.8% ya eneo la China.
Wastani wa urefu wa mwinuko
mkoani Tibet ni zaidi ya mita
4,000, hivyo inajulikana kwa
“Paa la Dunia”. Idadi ya wakazi
wa Tibet ni zaidi ya milioni
2.6, kati yake idadi ya watu
wa kabila la watibet ni milioni
2.5 ikichukua 96% ya jumla ya
idadi ya watu wa Tibet. Tibet
ni mkoa wenye idadi ndogo kabisa
ya watu nchini China, na pia
ni mkoa wa kwanza wenye idadi
ndogo ya wakazi kwenye eneo
la kilomita za mraba moja, ambalo
ni pungufu ya watu wawili kwenye
eneo la kilomita moja ya mraba.