Uwanda wa juu wa Qingzang una
umaalumu pekee wa kimaumbile,
ambao unachukua nafasi muhimu
katika nyanda za juu na milima
mikubwa, na kujulikana kwa “ncha
ya tatu ya dunia”.
Sababu za kuitwa “ncha ya tatu
ya dunia” kunatokana na kuinuka
juu kwake na hewa baridi inayohusika.
Wastani wa mwinuko wake ni mita
zaidi ya 4,000 juu ya usawa
wa bahari pamoja na milima mikubwa
iliyoko katika pembezoni mwa
uwanja wa juu.