Historia na Hali Yake ya Hivi Sasa
中国国际广播电台
 

Kabla ya kuzaliwa Yesu Kristu, mababu jadi wa watibet walioishi kwenye uwanda wa juu wa Qingzang walikuwa na uhusiano na watu wa kabila la wahan walioishi sehemu ya ndani ya China. Baada ya kupita miaka mingi, watu wa makabila mbalimbali walioishi kwenye uwanda wa juu waliungana na kuwa wa kabila la watibet.
Hali ya vurugu na ya mfarakano iliyoendelea kwa miaka zaidi ya 300 ilimalizika mwanzoni mwa karne ya 7. Shujaa wa watibet Songzanganbu alianzisha rasmi enzi ya Turufan na kufanya Lahsa kuwa mji mkuu wake, ambapo walijifunza mafanikio ya teknolojia ya kisasa ya uzalishaji mali na siasa na utamaduni wa enzi ya Tang na kudumisha uhusiano wa kirafiki na enzi ya Tang katika mambo ya siasa, uchumi na utamaduni.
Katikati ya karne ya 13 sehemu ya Tibet iliingizwa katika nchi ya China na ilitawaliwa na serikali kuu pamoja na kuwepo kwa mabadiliko ya enzi kadhaa.
Baada ya kuanzishwa enzi ya Qing utawala kwenye sehemu ya Tibet uliimarishwa zaidi na kuwa wa kisheria na kiutaratibu.
Baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949, serikali kuu iliamua kutekeleza sera ya kuikomboa Tibet kwa njia ya amani kutokana na historia na hali halisi ya huko. Serikali kuu ya umma ikifuata matarajio la watu wa Tibet ilifanya mageuzi ya demokrasia na kuvunja utaratibu wa kimwinyi katika Tibet, tokea hapo watumwa wa huko walipata uhuru na kutouzwa, kubadilishwa au kuwa mali ya matajiri ya kulipia madeni yao. Mkoa unaojiendesha wa Tibet ulianzishwa rasmi mwezi Septemba mwaka 1965.