Kabila la Watibet 

中国国际广播电台

      Kabila la watibet ni lenye idadi kubwa ya watu kwenye sehemu ya Tibet. Watibet wanashughulikia zaidi kazi za kilimo na ufugaji, wakati wakazi wa mijini wanashughulikia kazi ndogo ndogo za ufundi, uzalishaji bidhaa viwandani na biashara.
Watibet ni waumini wa dini ya kibudhaa ya kitibet. Watu wa kabila hilo ni wachangamfu na ni hodari sana kwa uwindaji na uchezaji ngoma. Watibet wanapenda kuvaa mashati yenye mikono mirefu; wanaume wanavaa kanzu kubwa nje, wanawake wanavaa kanzu isiyo na mikono na kufunga mkanda kiunoni, na wanawake walioolewa wanapenda kuvaa vitambaa vyenye rangi mbalimbali kama za upinde wa mvua. Wanaume kwa wanawake wanapenda kufuga nywele ndefu na kusuka mikia ya nywele na kupenda kuvaa mapambo ya hereni, bangili na pete. Chakula kikuu cha watu watibet ni unga wa mseto wa shayiri ya uwanda wa juu (highland barley) na choroko na kupenda kunywa chai ya samli na pombe na kula nyama za ng’ombe na kondoo.