Dini ya kibudha ya kitibet na mahekalu ya wa-lama
中国国际广播电台

     Dini ya kibudha ya kitibet imeenea kwenye sehemu ya Tibet na Mongolia ya ndani nchini China, wenyeji wa huko waliita dini hiyo kuwa ni “dini ya lama”, hii ni dini ya kibudha iliyoenea Tibet kutoka India na sehemu za ndani za China ambayo iliunganishwa na dini za kale za huko na kuwa dini yenye umaalum wa kitibet.

Kutokana na athari ya dini ya kibudha ya kabla ya wahan la China na dini ya kibudha ya India, mahekalu ya dini ya kibudha ya kitibet mengi yalijengwa kwa mtindo wa jengo la kifalme la kabila la wahan tena kuonesha mtindo wa kitibet, kwa kawaida, mahekalu hayo ni makubwa sana yenye taadhima, mapaa ya majengo huchongwa nakshi na kuchorwa picha ambayo yanaonekana ya kupendeza sana. Kwa mfano, Kasri la Budara la Lahsa, Hekalu la Drepung na Hekalu ya Tar la Qinghai yote ni majengo mazuri ya zama za kale.

Ujenzi wa mahekalu ya Tibet pia hutilia maanani zaidi kwa kuonesha taswira, ajabu na miujiza ya dini ya kibudha ya kitibet. Mahekalu ya kawaida huwa na ukumbi mkubwa na mrefu wa kuabubu sanamu za budhaa, ndani kupambwa na mapazia ya kidini ya rangi mbalimbali, nguzo za ukumbini hupambwa kwa mazulia za rangi, ndani kuna giza kidogo, hivyo watu wakiingia huko hujisikia ajabu ya dini.