Opera ya kitibet
中国国际广播电台

Opera ya kitibet ina historia ndefu tangu enzi na dahari, mitindo ya opera hiyo ni ya aina mbalimbali. Michezo ya Opera ya kitibet kama vile “Binti wa mfalme Wencheng” na “Mwana wa Mfalme Nosang” imekuwa michezo inayosifiwa na kupendwa na watu kwa miaka mingi tangu zamani, muziki wa michezo hiyo ni mwororo sana, vifuniko vya nyuso na mapambo ya nguo ya wahusika wa michezo hiyo ni ya rangi mbalimbali na kupendeza kiajabu. Yote hayo yameonesha msingi imara wa utamaduni kwenye opera ya kitibet.

Opera ya kitibet ni michezo ya sanaa inayoonesha nyimbo na ngoma za kienyeji. Toka karne ya 15, mtawa Tangdongjiebu wa madhehebu ya Geju alitunga michezo ya opera ya kitibet na kuongoza wachezaji kuonesha michezo ya nyimbo na ngoma iliyoeleza hadithi fupi katika sehemu mbalimbali. Baada ya miaka mingi, michezo ya opera ya kitibet imeendelea vizuri, michezo yenyewe ilitungwa kikamilifu na kusimulia hadithi nzuri na kuongeza vivutio mbalimbali pamoja na mapambo, mitindo tofauti ya uimbaji kwa kufuata bendi na uimbaji wa wanaoambatana, opera ya kitibet kweli ni michezo mbalimbali ya sanaa.

     Watibet wanapenda sana michezo ya opera ya kitibet, kila yanapofanyika maonesho ya michezo ya opera hiyo, watu wengi kutoka sehemu za mbali hata wanaweza kumiminikia kwenye uwanja mmoja kutazama maonesho.