Shirikisho Kuu la Wanawake wa China

Radio China Kimataifa
 

 Shirikisho hili ni jumuiya yenye uwakilishi mkubwa inayowashirikisha wanawake wa makabila mbalimbali na wa fani mbalimbali nchini China, chini ya uongozi wa chama cha kikomunisti cha China ili kujipatia ukombozi zaidi. Shirikisho Kuu la Wanawake wa China ni daraja la mawasiliano kati ya chama cha kikomunisti cha China na serikali ya China na wanawake, na ni moja ya mihimili muhimu ya jamii kwa utawala wa nchi. Shirikisho Kuu la Wanawake wa China lilianzishwa mwezi March mwaka 1949, mwanzoni liliitwa Shirikisho la Wanawake la Kidemokrasia la taifa la China. Mwaka 1957 lilibadilishwa jina na kuwa Shirikisho la Wanawake la Jamhuri ya Watu wa China, mwaka 1978 lilibadilishwa kuwa Shirikisho Kuu la Wanawake wa China. Jukumu lake la kimsingi ni kuwaunganisha na kuwahamasisha wanawake kushiriki katika ujenzi wa uchumi na maendeleo ya kijamii, kuwakilisha na kulinda maslahi ya wanawake na kuhimiza usawa kati ya wanaume na wanawake.