Harakati ya Kujenga Familia Bora za Kistaarabu
Radio China Kimataifa
 

Mashirikisho ya wanawake yalianzisha harakati za kuchagua familia bora za ustaarabu kuanzia miaka ya 50 ya karne iliyopita. Hadi mwishoni mwa mwaka 1999, familia karibu elfu 30 zilichaguliwa na kupewa sifa ya familia bora za ustaarabu za ngazi ya mkoa. Ili kuzisaidia familia kufuatana na jamii ya zama za hivi sasa inayobadilika siku hadi siku, kuhimiza njia ya maisha ya ustaarabu, afya na sayansi, mashirika ya wanawake nchini kote yamefanya shughuli za aina mbalimbali za utamaduni wa kifamilia. Kuwasaidia wakazi kuwa na mtazamo mzuri kuhusu maisha na thamani ya vitu. Zaidi ya hayo, mashirikisho ya ngazi mbalimbali ya wanawake pia yamewasaidia wakazi kujenga familia zenye masikilizano.

Katika sehemu za vijijini, China imeanzisha shughuli za kuwasaidia wakulima kuondokana na umaskini na kujiendeleza kwa njia za kisayansi na teknolojia. Kuwaongoza wakulima kuachana na desturi zinazopitwa na wakati, kuinua mwamko wao wa kujenga mwili na kuboresha mazingira, kuinua kiwango cha maisha kwa kuchapa kazi. Pia inaendelea kukamilisha miradi ya aina mbalimbali kama vile kutengeneza mabomba ya maji, mifereji, barabara, vyoo na vizuizi vya mifugo, ili kubadilisha sura ya familia na vijiji. Katika mitaa ya mijini, pia zimefanywa shughuli za aina mbalimbali kama vile, “naupenda mtaa wangu” na “naipenda familia yangu”, kuwakaribisha majirani nyumbani na kuwahimiza wakazi wanaokaa kwenye jengo moja wafahamiane, na kuongeza wajibu wa kijamii kwa wanafamilia. Mikoa kadhaa imeanzisha shughuli za kutoa elimu ya mazingira kwa kauli mbiu ya “wanawake, maskani na mazingira”, kueneza ujuzi wa hifadhi ya mazingira, kuinua mwamko wa hifadhi ya mazingira kwa familia zote, na shughuli za kusafisha na kuboresha mazingira ya mtaa, na kusukuma mbele ujenzi wa mtaa wa kistaarabu.