Radio China Kimataifa
Lin Qiaozhi
Mwanasayansi wa utibabu, mzaliwa wa mji wa Xiamen, mkoani Fujian. Alihitimu katika chuo Kikuu cha Utibabu cha Xiehe mwaka 1929 na kupata shahada ya udaktari ya tiba (M.D.) Yeye ni profesa na mkurugenzi wa idara ya uzazi ya Hospitali ya Xiehe, pia ni mkuu wa heshima wa Hospitali ya Uzazi ya Beijing, na naibu mkuu wa Taasisi ya Sayansi ya Utibabu ya China. Alifanya utafiti na kupata mafanikio makubwa kuhusu jinsi mimba inavyotungwa katika tumbo la uzazi na jinsi ya kutibu magonjwa ya wanawake na kadhalika, alikuwa na ustadi mzuri wa tiba na kufanya kazi nyingi katika uenezaji wa ujuzi wa kisayansi kuhusu afya za wanawake na watoto nchini China. mwaka 1995, aliteuliwa kuwa mwanataaluma.
Xie Xide
Yeye ni mwanafizikia, mzaliwa wa mji wa Quanzhou, mkoani Fujian. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Xiamen mwaka 1946. Mwaka 1951, alipata shahada ya udaktari ya fizikia katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Uhandisi cha Massachusetts na kubaki chuoni kuendelea na masomo ya baada ya shahada ya udaktari. Kwa nyakati tofauti alipata shahada ya heshima ya udaktari ya sayansi katika vyuo vikuu 12 vya Marekani, Uingereza, Canada, Japan na mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong. Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa mwanataaluma wa Taasisi ya Sayansi ya Dunia ya Tatu, mwanataaluma wa Taasisi ya Sayansi ya Marekani na profesa wa Chuo Kikuu cha Fudan cha Shanghai. Bibi Xie Xide alishughulikia hasa utafiti na ufundishaji kuhusu semiconductor ya fizikia, ramani ya nishati yabisi na kadhalika. Alipata matokeo kadhaa makubwa, pia alikuwa kiongozi wa utafati wa kisayansi wa sekta hizo. Mwaka 1980 aliteuliwa kuwa mwanataaluma wa Taasisi ya Sayansi ya China.
He Zehui
Mtaalamu wa fizikia ya nyuklia, mzaliwa wa mji wa Suzhou, mkoani Jiangsu, ukoo wake unatoka sehemu ya Lingshi, mkoani Shanxi. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Qinghua mwaka 1936. Mwaka 1940 alipata shahada ya udaktari ya uhandisi katika Chuo Kikuu cha Viwanda cha Berlin, Ujerumani. Yeye aliwahi kuwa mtafiti wa fizikia ya nishati ya juu katika Taasisi ya Sayansi ya China. Alipata mafanikio makubwa katika sekta ya fizikia duniani na kutoa mchango mkubwa katika ujenzi wa maabara, vituo vya ukaguzi wa ulimwengu na puto la anga la juu, na kufanya utafiti kuhusu fizikia ya anga ya nishati ya juu. Mwaka 1980 aliteuliwa kuwa mwanataaluma wa Taasisi ya Sayansi ya China.
Jiang Lijin
Mtaalamu wa kemikali, mzaliwa wa mji wa Beijing. Sasa ni mtafiti wa idara ya utafiti wa kemikali ya Taasisi ya Sayansi ya China. Mwaka 1946 alihitimu na kupata shahada ya pili katika kitivo cha kemikali cha Chuo Kikuu cha Furen. Mwaka 1951 alipata shahada ya udaktari katika Chuo Kikuu cha Minisuda cha Marekani, aliwahi kufanya kazi ya utafiti katika vyuo vikuu vingine vya Marekani. Mwaka 1955 alirudi nchini China. Miradi yake miwili ya utafiti kuhusu dawa za mitishamba na muundo wa mimea ya majini ilipata tuzo ya nafasi ya pili ya sayansi ya kimaumbile kwa nyakati tofauti katika miaka ya 90. Mwaka 1980, aliteuliwa kuwa mwanataaluma wa Taasisi ya Sayansi ya China.
Yin Wenying
Mtaalamu wa elimu ya wadudu. Mzaliwa wa sehemu ya Pingxiang mkoani Hebei. Alihitimu masomo kutoka kitivo cha elimu ya viumbe cha Chuo Kikuu cha Zhongyang. Yeye ni mtafiti wa idara ya utafiti wa wadudu ya Shanghai ya Taasisi ya sayansi ya China. Aliwahi kuandika makala nyingi za kitaaluma kuhusu elimu ya wadudu, aliteuliwa kuwa mwanataaluma wa Taasisi ya Sayansi ya China mwaka 1991.
|