Sheria na Kanuni za Kulinda Haki na Maslahi ya Wanawake
Radio China Kimataifa
 

Hivi sasa China imeanzisha mfumo wa kisheria wa kulinda haki na maslahi ya wanawake na kuhimiza usawa kati ya wanaume na wanawake kwa msingi wa katiba. Sheria hizo ni pamoja na "sheria ya raia", "sheria ya makosa ya jinai", "sheria ya upigaji kura", "sheria ya kazi", "sheria ya ndoa", "sheria ya idadi ya watu na uzazi wa mpango", "sheria ya kusaini mkataba wa kulima mashamba" na kadhalika. Tokea "sheria ya kuhakikisha haki na maslahi ya wanawake ya Jamhuri ya Watu wa China" itolewe mwezi Aprili mwaka 1992, Bunge la Umma la China limetunga sheria 12 na maazimio mawili husika ya kulinda haki na maslahi ya wanawake, kama vile "sheria ya kazi", "sheria ya kuchagua kamati ya wanavijiji", "sheria ya kuhakikisha haki na maslahi ya wazee", "sheria ya idadi ya watu na uzazi wa mpango" na "sheria ya kusaini mkataba wa kulima mashamba".

Wakati huo huo, China pia imerekebisha sheria 7 zinazohusiana na haki na maslahi ya wanawake kama vile "sheria ya upigaji kura", "sheria ya makosa ya jinai" na "sheria ya ndoa". Baraza la serikali limetunga sheria na kanuni 7 kuhusu kulinda haki na maslahi ya wanawake, na idara nyingine husika zimetunga kanuni 98 husika. Mikoa na miji yote imechukua hatua za kutekeleza sheria hizo. Ili kuhimiza utekelezaji wa sheria hizo, idara husika na sehemu mbalimbali pia zimetunga nyaraka za sera, na kuanzisha harakati za kueneza sera hizo ili watu wote wafahamishwe jinsi ya kulinda haki na maslahi ya wanawake.