Haki ya Wanawake wa China ya Kupewa Ajira
Radio China Kimataifa
 

Ili kuwahakikishia wanawake haki ya kupewa ajira, idara husika za China siku zote zinatekeleza kwa bidii “sheria ya kazi”, kupiga marufuku ubaguzi wa kijinsia wakati wa kuajiri watumishi; kuwahakikishia wanawake wawe na haki ya kumiliki mali na ufundi sawa na wanaume, kuhakikisha kuwa wanaume na wanawake wanafanya kazi ya aina moja na kupata mshahara sawa, kupunguza pengo la mapato kati ya wanaume na wanawake; na kupanua maeneo ya kuwaajiri wanawake. Kukuza shughuli za utoaji huduma ili kuongeza nafasi za ajira kwa wanawake; kutekeleza vizuri sera ya kulinda kazi ya wafanyakazi wanawake, wanawake wa vijijini wana haki sawa na wanaume katika kusaini mkataba wa kulima mashamba, kuendesha uzalishaji, na kupewa ardhi ya kujenga nyumba, kuwaelekeza na kuwasaidia wanawake wa vijijini wajifunze ufundi wa kikazi ili waweze kufanya shughuli nyingine licha ya kilimo.