Haki ya Wanawake ya Kupata Elimu
Radio China Kimataifa
 

"Katiba", "sheria ya kutoa elimu ya lazima", "sheria ya kuhakikisha haki na maslahi ya wanawake" na sheria nyingine za China zote zina vifungu vinavyoeleza kuwa, wanawake wana haki sawa na wanaume ya kupata elimu. Mwaka 2001, asilimia 99.1 ya watoto wa China wenye umri wa kwenda shule walipata nafasi ya kwenda shule, ambapo asilimia 99.01 ya watoto wa kike walipata nafasi ya kwenda shule, Mwaka 2002, wanafunzi wa kike walichukua asilimia 46.7 ya wanafunzi wote wa shule za sekondari, ambapo kiasi cha wanafunzi wa kike katika vyuo vikuu kilichukua asilimia 44. Katika miaka ya hivi karibuni, kiwango cha wanawake wa China cha kupata elimu kimeinuka sana, na tofauti kati ya wanaume na wanawake katika kupata elimu inapungua siku hadi siku. Kutokana na takwimu ya sensa ya 5 iliyofanyika mwaka 2000, wanawake wa China kwa wastani walipata elimu ya miaka 7.07, tofauti ya kupata elimu kati ya wanawake na wanaume ilipungua kufikia mwaka 1.07 kutoka ile ya 1.40 ya mwaka 1995.