Haki na maslahi sawa ya wanawake katika ndoa na familia
Radio China Kimataifa
 

Kati ya familia milioni 350 za China, familia nyingi zinaundwa kutokana na ndoa halali ya kujiamulia kwa msingi wa kupendana, uhusiano kati ya wanaume na wanawake katika familia ni sawa na kusikilizana, wanawake wana uhuru na haki juu ya mali.

Mwezi Aprili mwaka 2001, Halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China ilitoa sheria mpya ya ndoa. Sheria hiyo inapiga marufuku kuwa na wake au waume wawili, ni haramu kwa mtu mwenye mke au mume kuishi pamoja na mwingine, kupiga marufuku kufanya vitendo vya kimabavu nyumbani, kuweka utaratibu kuhusu ndoa ambazo hazitambuliki, kukamilisha utaratibu wa kugawa mali za familia kati ya mume na mke, kuweka utaratibu wa kufidia hasara kutokana na talaka na vitendo vya kimabavu nyumbani, kuhukumu vitendo vya kuharibu ndoa na familia ili kulinda hadhi ya wanawake katika familia.

Ili kuanzisha uhusiano wa kindoa na kifamilia wenye usawa, masikilizano na ustaarabu, China imeunda kikundi cha kuratibu shughuli za kujenga familia bora cha China kilichoundwa pamoja na mashirika 18 ya serikali na yasiyo ya serikali, na kuzifaya shughuli za kujenga familia bora katika mpango mkuu wa maendeleo ya uchumi na ujenzi wa ustaarabu. Mwaka 2000 matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Shirikisho Kuu la Wanawake la China na Idara ya Utoaji Takwimu ya China yalionesha kuwa, asilimia 93.2 ya wanawake wa miji na vijiji waliona kuridhika na hali yao ya ndoa.