Hali ya Jumla ya Maingiliano Kati ya Wanawake wa China na wa Nchi za Nje
Radio China Kimataifa
 

Tokea mwezi Juni mwaka 1995 Shirikisho Kuu la Wanawake la China likiwa jumuiya ya kwanza isiyo la kiserikali ya China kupata hadhi ya kushiriki katika mikutano ya Umoja wa Mataifa, limeshiriki kwa juhudi katika shughuli za Umoja wa Mataifa na za pande nyingi za kimataifa, limetuma wajumbe kuhudhuria mikutano mingi ya Umoja wa Mataifa, kama vile mkutano wa kamati ya haki za binadamu, mkutano wa kamati ya hadhi ya wanawake, mkutano maalum wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la wanawake na la watoto, na mkutano wa wakuu wa dunia kuhusu suala la maendeleo endelevu. Shirikisho Kuu la Wanawake la China limetoa sauti na mchango katika kulinda amani ya dunia na maslahi ya nchi zinazoendelea na maendeleo ya harakati za wanawake duniani.

Mashirikisho ya wanawake ya China yamefanya maingiliano na ushirikiano na nchi za nje kwa njia mbalimbali. Hivi sasa Shirikisho Kuu la Wanawake la China limeanzisha uhusiano wa kirafiki na mashirikisho 700 ya wanawake na watoto ya nchi 151, kujishirikisha mambo ya wanawake ya Umoja wa Mataifa na ya pande nyingi, lilifaulu kuandalia mkutano wa 4 wa wanawake wa dunia na mkutano wa kubadilishana maarifa wa mkutano huo, kongamano la wanawake kati ya China na Umoja wa Ulaya na mkutano wa viongozi wanawake wa Shirika la Ushirikiano wa Uchumi la Asia na Pasifiki APEC. Mashirika ya wanawake ya China pia yamefanya ushirikiano wa kimataifa ili kuwahudumia vizuri wanawake na watoto wa China, yamekuwa mashirika ya wanawake yanayojulikana duniani.