Nadharia ya Msingi wa Tiba ya Kichina
中国国际广播电台

       Nadharia ya msingi wa tiba ya kichina ni ujumlisho wa nadharia kuhusu uhai wa miili ya binadamu pamoja na kanuni ya mabadiliko ya maradhi.

Hasi na Chanya ni za eneo la falsafa ya kale nchini China. Watu waliweka hali ya mgongano katika eneo la hasi na chanya na kueleza mabadiliko ya vitu kwa kutumia mvutano kati ya hasi na chanya. Nadharia hiyo inasema kuwa uwiano mwafaka kati ya hasi na chanya ni msingi wa kudumisha hali nzuri ya miili ya binadamu, pindi uwiano huo ukivurugika binadamu ataugua.

Elimu ya “wuxing” ni elimu inayoeleza uwezo na uhusiano kati ya viungo vya mwili wa binadamu kwa maeneo matano ya falsafa ya mti, moto, udongo, dhahabu na maji, inasema kuwa endapo uwiano kati ya viungo vya mwili utavurugika, binadamu ataugua.