Tiba za Jadi za Kabila la Watibet
中国国际广播电台

HALI YA TIBA ZA KITIBET

Tiba za kitibet ni moja ya sehemu muhimu ya tiba za jadi za kichina, ambayo imevumbuliwa katika uzoefu wa muda mrefu wa kutibu wagonjwa katika maeneo ya makabila madogo madogo ,hususan katika maeneo ya kabila la watibet ikiwemo ya mikoa ya Tibet, Qinghai, Sichuan na Gansu, licha ya hayo tiba za kitibet pia zimeenea sana katika nchi za Asia ya kusini zikiwemo India na Nepal. Kutokana na mazingira maalumu ya jamii na maumbile, dawa za kitibet zinatumia zaidi wanyama na mimea ya sehemu za baridi kali na zenye hewa kidogo.

Katika tibet, kutokana na kuwa mawazo ya kidini yameingia katika pande mbalimbali za jamii na kuwa nguvu kubwa inayoongoza, hivyo tiba za kitibet zinaingiliana na dini ya Buddha ya kitibet tangu ilipoanza kuweko.

NDAHARIA YA KIMSINGI YA TIBA ZA KITIBET

Katika uzalishaji mali, maisha na uzoefu wa tiba, tiba za kitibet zimekuwa na mfumo wake wa kipekee wa nadharia.

Nadharia ya chimbuko tatu

Nadhari ya tatu za kitibet inaona kuwa mwilini mwa binadamu kuna chimbuko tatu za “Long”, “Chiba” na “Beigen”; Msingi wa vitu vya aina 7 ambavyo ni rutuba ya chakula, damu, shahamu, mifupa, ute ulioko katikati ya mifupa na shahawa; Vinyesi vya binadamu vikiwa ni pamoja na kinyesi cha haja kubwa, kinyesi cha haja ndogo na jasho. Chimbuko tatu zinatawala msingi wa vitu vya aina saba pamoja na mabadiliko ya vinyesi vya aina tatu. Katika hali ya maisha ya kawaida mambo hayo matatu yanategemeana na kuzuiana, hali ambayo inaleta mazingira ya kupatana na kuendana. Wakati moja au zaidi ya moja ya mambo hayo matatu yakiingia kwenye hali ya kustawi au kuzorota kutokana na sababu fulani, unaweza kutokea ugonjwa wa “Long”, “Chiba” au “Beigen”, tiba zinatakiwa kuyarekebisha uhusiano wa mambo hayo matatu na kuyarejesha katika hali ya kupatana.

UMAALUMU WA TIBA ZA KITIBET

TIBA ZA MADAWA

Wakati inapotibu mgonjwa, tiba za kitibet huwa zinatumia kitu kinachoongoza dawa kwenda katika sehemu yenye matatizo, kwa mfano wakati mwingi sukari inatumika kuongoza dawa katika kuponya mgonjwa mwenye homa, na kutumia sukari ya guru (sukari nyeusi) kutibu mgonjwa aliyeugua kutokana na kupatwa na baridi.

Mbali na hayo, namna ya kumeza dawa pia kuna kanuni zake. Kwa mfano donge la dawa kwa kawaida linasindikizwa na maji, lakini mgonjwa aliyeugua kutokana na baridi, anatakiwa kusindikiza dawa kwa maji moto; kwa mgonjwa yanayotokana na joto, basi atafanya kinyume chake na kusindikiza dawa kwa maji baridi.

MBINU YA UTAPISHAJI

Mbinu ya kufanya mgonjwa kutapika kwa kumpa dawa ya utapishaji ni moja ya tiba za kitibet, ambayo inaweza kutibu matatizo ya chakula kubaki kwenye utumbo wa chakula, kula chakula chenye sumu kwa bahati mbaya au wadudu walioko ndani ya matumbo ya binadamu walijisogeza karibu na koo na kushindwa kurejea ndani au kwa tatizo la kuwa na makohozi kooni, isipokuwa wadhaifu, wazee, wajawazito pamoja na watoto wachanga. Kwa watu wale waliokula vitu vyenye sumu, muda mrefu ukipita muda mrefu, wasitapishwe kwa kula dawa, kwani vitu vyenye sumu haviko tena katika utumbo wa chakula.

MBINU YA UPAKAJI WA DAWA

Kutumika dawa ya kupaka ni moja ya mbinu rahisi ya tiba za kitibet, hata watu wa kawaida wanaweza kuitumia. Tiba za kitibet zinaona kuwa upakaji wa dawa, ambayo ni ya aina ya mafuta, unaweza kutibu udhaifu wa mwili, kuchoka kupita kiasi na kuwa una usingizi sana.

TIBA YA KUOGA KWA MAJI YENYE DAWA

Mbinu ya kuoga kwa maji yenye dawa ni moja ya tiba ya kitibet. Maji yanayotumika zaidi ni ya chemchem yenye madini ya sulfur.