Tiba za Kimongolia
中国国际广播电台

HALI YA TIBA ZA KIMONGOLIA

Tiba za kabila la wamongolia nchini ziliendelezwa hatua kwa hatua kuwa tiba za jadi za kimongolia katika uzoefu wa tiba katika miaka mingi iliyopita, na pia ni sayansi ya tiba inayoendana na umaalumu wa kikabila na mazingira ya huko. Tiba za kimongolia zinajulikana kwa kutumia dawa kidogo na zenye ufanisi mwingi, rahisi kutumika na ya gharama ndogo.

NADHARIA YA MSINGI WA TIBA ZA KIMONGOLIA

Tiba za kimongolia zinatumia uhusiano za chimbuko tatu za “Heyi”, “Xila” na “Badagan” kufafanua hali ya mwili na kuugua ugonjwa kwa binadamu. “Heyi” ni nguvu ya uwezo wa mwili wa binadamu. Mawazo, maneno, vitengo na kazi za maungo ya mwili vyote vinatawaliwa nayo. Endapo “Heyi” haifanyi kazi zake barabara, uwezo wa maungo ya mwili wa binadamu utafifia na kuonekana kutokuwa na umakini, kupaa usingizini na kuwa msahaulifu.

“Xila” maana yake ni moto. Ujoto wa mwili, viungo vya mwili pamoja na nguvu ya kuchangamka vyote vinahusika na “Xila”. “Xila” ikionekana kuwa na nguvu kubwa zaidi, binadamu huwa na homa au mwepesi kukasirika. “Badagan” ni kitu kama ute mwilini mwa binadamu kikionekana kuwa baridi. Pindi “Badagan” haifanyi kazi sawasawa, binadamu ataonekana kuwa baridi na kuwa na ute mwingi.

TIBA MAALUMU ZA KIMONGOLIA

TIBA ZA KUTOA DAMU

Kupasua au kutoboa mshipa wa damu inayorudi kwa moyo ili kutoa damu yenye matatizo.

TIBA YA KUFYONZA NGOZI KWA CHUPA

Tiba hiyo hufanyika kwa chupa ya kufyonza ngozi ya mwili kwa chupa na kutoa damu kwa pamoja. Kwanza kuchagua sehemu moja ya kufyonza ngozi, baada ya kuondolewa chupa ya kufyonza, kutoboa ngozi iliyoinuka ya sehemu hiyo kwa sindano, kisha kutumia chupa ya kufyonza tena ili kutoa damu yenye matatizo pamoja na maji ya rangi ya manjano. Tiba hiyo inaleta matokeo haraka wala haina uchungu na hatari.

Mbali na hayo, tiba za kimongolia kuna mbinu nyingine za kuwaponya wagonjwa zikiwa ni pamoja na kutumia maziwa ya farasi yaliyoumuka (kwa hamira), akyupancha na kumia mikono kurejesha mfupa ulioteguka.