Tiba za Jadi za Kikorea
中国国际广播电台

HALI YA TIBA ZA KIKOREA

Tiba za jadi za kikorea ni mfumo wa tiba za jadi zilizoanzishwa juu ya msingi wa utamaduni wa kikorea na kujumuisha uzoefu wa kuzuia maradhi na kutibu wagonjwa. Toka zamani za kale, kabila la wakorea lilikuwa maingiliano ya kirafiki ya muda mrefu na kabila la wahan, utamaduni na tiba za makabila hayo mawili pia yaliingiliana tokea zamani.

CHANZO CHA TIBA ZA KIKOREA

Tiba za kikorea zina sehemu mbili ambazo ni dawa za kabila la wahan na dawa za kikorea.

Kutokana na kuwa tiba za kikorea zimeingiza elimu ya tiba na dawa za jadi za kichina, hivyo tiba za kikorea zinatumia dawa za jadi za kichina kama silaha za kabila la wakorea kupambana na maradhi. Kwa mfano, kitabu kijulikanacho kwa “Dawa za Sixiang”, dawa zote zilizoelezwa ni za kichina ambazo ni za aina 271, na dawa zilizoelezwa katika kitabu kijulikanacho kwa “Tiba za Mashariki” ni za makundi makubwa 15 zenye aina zaidi ya 1,400.

Matumizi ya dawa za kabila la wakorea yamekuwa na historia ya miaka mingi, hususan baada ya mwaka 1949 matumizi ya dawa zilizokuwa zinatumika na wakorea kutibu wagonjwa zilikusanywa na kuandikwa katika kitabu cha dawa.